TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA MPANGO WA TAIFA WA KUJIANDAA NA KUKABILIANA NA MAAFA NA MKAKATI WA TAIFA WA MAWASILIANO WAKATI WA MAAFA.

Msemaji kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Julian Tendwa akieleza kwa Waandishi wa Habari juu ya Mpango wa Taifa wa Kujiandaa na Kukabiliana na Maafa (kushoto),akiwa na Zamaradi kawawa ambaye ni Afisa habari wa idara ya habari maelezo (kulia).
Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam, msemaji kutoka Ofisi ya waziri amesema ya kuwa, Ningependa ifahamike kuwa Maafa ni matokeo ya janga ambalo huathiri kwa kiwango kikubwa mfumo wa kawaida wa maisha ya jamii kwa kusababisha vifo, majeraha, upotevu au uharibifu mkubwa wa mali au mazingira ambayo jamii iliyoathirika isipokuwa imejiandaa na maafa haiwezi kuyakabili maafa kwa uwezo au rasilimali zake bila msaada kutoka nje ya jamii hiyo.
Aidha, amesema hayo leo Kwa kuzingatia hayo Serikali kupitia Idara yake ya Uratibu wa Maafa imeandaa Mpango wa Taifa wa Kujiandaa na Kukabiliana na Maafa unaoainisha majukumu ya Wadau mbalimbali, kwa ajili ya kuhakikisha kunakuwa na ufanisi katika jamii nzima kwa kuwa na uelewa mkubwa wa kujiandaa, kukabili na kupunguza athari za maafa nchini.
No comments
Post a Comment