WASANII WAKABIZIWA NYUMBA MKURANGA
Na Kasali Mgawe
Vifijo na nderemo vilisikika kwa wingi wilayani mkuranga
mkoa wa pwani baada ya kufanyika tukio kubwa la kuwakabizi nyumba wasanii 38 wanachama
wa mtandao wa wasanii Tanzania (SHIWATA)
Tukio hilo lililovutia wakazi wa eneo la mkuranga na vijiji
vya jirani liliweza kuwakutanisha wasanii ,waandishi wa habari na wanamichezo
ambao kwa pamoja walipata burudani mbalimbali za ngoma maigizo na sarakasi.
MGENI RAMSI AFISA TRAFA YA SHUNGUBWENI CLEMENT MUYA AKITOA HUTUBA KATIKA SHEREHE HIYO ALIMUWAKILISHA MKUU WAWILAYA YA MKURANGA |
MMOJA WA WASANII WALIOKABIDHIWA NYUMBA AKIONYESHA CHETI CHAKO CHA UTAMBUZI |
MWENYEKITI WA SHIWATA KASIMU TAALIBU AKITOA HUTUBA KATIKA SHEREHE HIZO |
MKUU WA WILAYA YA MKURANGA MSTAAFU AKITOA HENRY CLEMENSE AKIZUNGUMZA KATIKA SHEREHE HIZO |
NYUMBA MOJA WAPO YA KISASA ILIYOKABIDHIWA KATIKA SHEREHE HIZO |
WASANII WALIOKABIDHIWA NYUMBA ZAO WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA VIONGOZI WA SHIWATA NA MGENI RASMI ALIYEMUAKILISHA MKUU WA WILYA MKURANGA |
BAADHI YA NYUMBA ZILIZOKABIDHIWA KWA WASANII WANACHAMA WA SHIWATA KATIKA KIJIJI CHA MWANZEGA MKURANGA |
MCHEZAJI WA ZAMANI WA TAIFA STARS JERRY MTAGWA AKIKABIDHIWA CHETI NA NYUMBA KUTOKA KWA MGENI RASMI |
MMOJA WA WASANII AKIKABISHIWA NYUMBA YAKE NA CHETI CHA UTAMBUZI NA MGENI RASMI |
BAADHI YA WASANII WAKITUM,BUIZA KATIKA SHEREHE HIZO |
Akizungumza katika tukio hilo afisa tarafa ya shungubweni Mkuranga ndugu Clement Muya ambaye alimuwakilisha mkuu wa wilaya ya mkuranga
alisema kuwa SHIWATA imefanya jambo kubwa kwa wasanii kwa kuweza kuwaunganisha
na kuchukua maeneo ili waweze kujenga na kufanya shughuli za kilimo
Bwana Muya aliongeza kuwa ni muhimu kwa wasanii
wajitambue na kujiweka mbali na mambo
yasiyofaa katika jamii kama utumiaji wa dawa za kulevya na wajiunge kwenye
mtandao wa wasanii wenye lengo la kusaida wasanii hapa nchini kuwa na maisha na
makazi bora.
Wakati huo mkuu wa wilaya ya mkuranga mstaafu Henry Omuya
Clemense ambaye alikuwa mgeni mualikwa
katika sherehe hiyo alisema kuwa SHIWATA imeweza kutekeleza mpango wake wa kuwaunganisha
wasanii na kuwajengea misingi mizuri ya maisha kwa kuwa na makazi bora.
Mkuu wa wilaya huyo mstaafu aliongeza kuwa SHIWATA imeleta mabadiliko kwa wakazi wa mkuranga
kwani kwa kupita mipango yao huduma za jamii zitaongezeka kama vile huduma
za maji na shule katika eneo hilo.
Akizungumza wakati wa kumkaribisha mgeni rasmi mwenyekiti wa
mtandao wa wasanii tanzania (SHIWATA) mwalimu Cassim Talib alisema wamejipanga
kuwasaidia wasanii kuweza kutoka katika wimbi la umasikini kwa kuwaandalia
mazingira mazuri ya maisha yao.
Mwenyeki ti huyo alisema kuwa wanachama zaidi ya 200
wamechangia ujenzi wa nyumba hizo na wanachama 38 ndiyo walimaliza michango yao
na kuweza kukabidhiwa nyumba hizo zenye thamani tofauti kutokana na uchangiaji
wake.
Akitoa shukrani kwa niaba ya wasanii wenzake waliokabidhiwa
nyumba hizo ndugu Jerry Mtagwa ambaye ni mchezaji wa zamani wa Taifa Stars alisema
kuwa anashukuru sana SHIWATA kwa kumuwezesha kuweza kumiliki nyumba hiyo kwani
itakuwa ni msaada mkubwa kwa yeye familia yake.
Mtwagwa ametoa wito kwa wasanii wengine wajiunge na SHIWATA ni kimbilio la wasanii na itakuwa msaada wa
mkubwa kwa maisha ya sasa na ya baadae kwani asalimia kubwa wanaishi katika
dimbwi kubwa la umasikini.
No comments
Post a Comment