SELF YAWAPA TEYO SACCOS THAMANI ZA OFISI
NA SELEMAN HAMAD
Mradi wa self uliyo chini ya wizara ya Fedha imeipatia fenicha za ofisini chama cha kuweka na kukopa cha vijana Temeke (TEYO SACCOS)
Fenicha hizo za ofisi ni viti vinne na meza mbili akizungumza katika ofisi ya Teyo Saccos hii leo baada ya kuleta vifaa hivyo afisa wa Self Lungu Phares alisema wametoa fenicha hizo kwa ajili ya kuboresha Saccos ya vijana temeke ili kuhakikisha inakuwa bora kiutendaji
Pia Lungu aliongeza kuwa wanampango wa kuongeza vifaa vingine vya ofisi kama komputa printa,benchi la wageni ,safe ya kuweka fedha,kabati la mafaili ,mabango n.k.
vilevile Lungu amewataka vijana wa Temeke kuwa mstari wa mbele kujiunga kwa wingi katika Saccos hiyo kwa kuwa ndio itakuwa mkombozi kwa wanyonge kwa kuweza kupatiwa mikopo yenye masharti nafuu kuweza kuboresha biashara zao .
MJUMBE WA KAMATI YA MIKOPO BWANA ISMAIL KASIMU AKIWA KATIKA OFISI TEYO SACCOS NA HIVYO NI BAADHI YA VIFAA VILIVYOTOLEWA NA MRADI WA SELF |
BAADHI YA VIFAA VILIVYOTOLEWA NA MRADI WA SELF KWA OFISI YA TEYO SACCOS LEO |
Akizungumza katika makabidhiano hayo katibu wa Teyo Saccos Kasali Mgawe alisema kuwa mradi wa SELF umekuwa msaada mkubwa kwa vijana baada ya kufanikisha upatikanaji wa Saccos ya hiyo na ukarabati wa ofisi na kupatiwa vifaa vya ofisi.
"tunashukuru sana serikali kupitia mradi wa Self kutuwezesha vijana kujikomboa kiuchumi kupitia Saccos hii ya vijana kwani itasaidia vijana wajasiliamali kujiendeleza biashara zao na kuboresha uchumi wa nchi " aliongeza Mgawe.
TEYO SACCOS kufikia mwezi huu imeweza kukupesha wanachama kumi na saba (17) kiasi cha zaidi ya milioni tatu kwa wanachama wao walioweza kukidhi vigezo vya kuwa na hisa,akiba na walijiunga uanachama kwa kipindi kisichopungua miezi mitatu.
TEYO SACCOS inapatikana katika mtaa wa bora kata ya chang'ombe jengo la shule ya chekechea chang'ombe karibu na ofisi za NIDA za wilaya ya Temeke au unaweza kupiga simu namba 0714807448,0714133283 na 0715613470
No comments
Post a Comment