Zinazobamba

JESHI LA POLISI KANDA MAALUMU WABAINI KUWA KIFAA KILICHODHANIWA NI BOMU KATIKA USHARIKA WA KIJITONYAMA KUMBE SI BOMU

Kutokana na taarifa, askari wa upelelezi wakiongonzwa na Mkuu wa Upelelezi kanda maalumu Dar es salaam ACP. Ahamed Msangi walienda katika kanisa hilo na kukuta kifaa hicho kilichodhaniwa ni Bomu kikiwa kinaning’inia katika transforma hiyo, kifaa hicho kilikuwa katika umbo la box dogo ambapo ndani yake kulionekana kuna betri na electonic saket, vifaa vya ndani ya radio, kikiwa kimezungushiwa cover lenye maandishi yafuatayo GPSNDE M2K2DC. Pia kulikuwa na maandishi ya kalamu ya wino yaliyosomeka TMA na AIRPOT.
DSC02779 (FILEminimizer)
Akizungumza na Waandshi wa Habari Jijini Dar es Saalaam Bw. Suleiman Kova, ambaye ni kamishina wa polisi wa kanda maalum amesema kuwa baada ya uchunguzi wa awali polisi walibaini kuwa kifaa hicho si bomu na ndipo walipokiondoa eneo lile na kwenda kukifanyia uchunguzi zaidi. Pia katika uchunguzi huo uliowashirikisha maofisa wa mamlaka ya hali ya hewa (TMA) ilibainika kuwa kifaa hicho si bomu bali ni moja ya vifaa vinavyotumika na mamlaka hiyo katika kuchunguza hali ya hewa ya anga za juu.
DSC02785 (FILEminimizer)
Kamishina wa Polisi kanda maalum Suleiman Kova akiwa amenyanyua juu kafaa ambacho kilidhaniwa kuwa ni bomu kumbe si bomu bali nikifaa ambacho kinachunguza hali ya anga za juu.


DSC02792 (FILEminimizer)
Bw. Agustino Nemba, ambaye ni mtaalamu tabiri wa mamlaka ya hali ya hewa ya anga za juu akiwa anaelezea kiufundi zaida na kiufanisi zaidi juu ya kifaa hicho ambacho kilihisiwa kuwa ni bomu.

PIA WAKATI HUOHUO JESHI LA POLISI KANDA MAALUM KWA KUSHIRIKIANA NA KAMPUNI YA SIMU YA MKONONI  ILI KUIMARISHA USALAMA WA JIJINI.
DSC02799 (FILEminimizer)
Amesema hayo kuwa katika utekelezaji wa maboresho kwa kushirikiana na wadau mbalimbali limeamua kutumia teknolojia ya kisasa kwa ajili yakusaida udhibiti uhalifu. Amesema kuwa hivi karibuni kumekuwa na vitendo vingi vya ujambazi wa kutumia silaha kwa watu hasa wafanya biashara kutoa pesa benki kwenda katika biashara zao.  Kutokana na usafirishaji huo ambao siyo salama jeshi la polisi limekubaliana na baadhi ya kampuni za simu ambazo pia zinajihusisha na utumaji, uhamishaji wa fedha kwa njia za elektronia ambayo ni ya kisasa na kimataifa,k wa kutumia mbinu hiyo mbadala sasa wafanya biashara hao wataweza kupokea fedha na kutuma bila kuzibeba eneo moja kwenda lingine. Pia Kamishina huyo amesema kuwa katika huduma hiyo tumeanza na kampuni ya Vodacom Tanzania kuanza kutoa elimu hususani kwa wafanya biashara.

No comments