Zinazobamba

WATU MILIONI 2.9 KUCHUKULIWA ALAMA ZA VIDOLE, PICHA


………………………………………………………………………………………
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imeanza zoezi la uchukuaji alama za vidole, picha na saini za kielekroniki kwa waombaji wa Vitambulisho vya Taifa katika mkoa wa Dar es Salaam ambapo watu wapatao milioni 2,900,000 wanatarajiwa kupatiwa huduma hiyo.
Zoezi hili lilianza Julai 15 katika wilaya ya Temeke ambayo imegawanywa katika kanda tano, itafuatiwa na Wilaya ya Ilala na kuhitimishwa na Kinondoni.
Kila Wilaya imegawanywa katika kanda, ili kuhakikisha wananchi wanahudumiwa vizuri na kurahisisha zoezi kwa kuwapunguzia wananchi usumbufu wa kukaa muda mrefu kusubiri katika foleni.
Zoezi la uchukuaji alama za vidole linakwenda sambamba na ujazaji fomu kwa waombaji wapya ambao hawakupa fursa ya kujaza fomu wakati wa zoezi la ujazaji fomu za maombi ya vitambulisho vya Taifa.
Waombaji wanatakiwa kufika kwenye vituo vya usajili na nyaraka halisi za kuthibitisha uraia na umri mathalan, cheti cha kuzaliwa, pasipoti, vyeti vya elimu ya msingi na sekondari, leseni ya udereva, kitambulisho cha bima ya afya na kitambulisho cha mpigakura.
Zoezi la Utambuzi na Usajili wa watu lina hatua mbalimbali ambazo zinatakiwa kufuatwa kwa lengo la kuweza kukusanya taarifa sahihi kwa lengo la kutumika na mifumo mingine. Hatua hizo ni kama ifuatavyo:-
    1. Ujazaji wa fomu za Utambuzi na Usajili;
    1. Uhakiki wa awali wa fomu za maombi;
    1. Uingizaji wa taarifa kwenye mfumo wa kompyuta;
    1. Kuthibitisha taarifa za mwombaji zilizo katika mfumo wa kompyuta;
    1. Uchukuaji wa alama za vidole, picha na saini ya kielektroniki;
    1. Utengenezaji wa Daftari Kuu la Taarifa za Watu;
    1. Uhakiki wa mwisho;
    1. Uchapishaji na Ugawaji wa Vitambulisho.
Mfumo huu una faida kubwa sana kwa taifa hili, hususan katika nyanja za kiuchumi kijamii na kiulinzi. Baadhi ya faida hizo ni kama ifuatavyo:-
    1. Kumtambua Mtanzania, mgeni na mkimbizi
    1. Kusidia katika kuongeza wigo wa ukusanyaji kodi ya Serikali kwa njia ya kuwatambua wachangiaji wengi zaidi
    1. Kuondoa wafanyakazi hewa katika Mfumo wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara Serikalini
    1. Kusaidia suala la utambuzi hususan kwenye mabenki na hivyo kuwasaidia wananchi kupata mikopo kwa urahisi zaidi

PINDA AFUNGUA KONGAMANO LA UWEKEZAJI MANYARA


IMG_0179Baadhi ya  washiriki wa  Kongamano la Kwanza la  Uwekezaji  katika Mkoa wa Manyara  wakimsikiliza  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati alipofungua   kongamano hilo mjini Babati  Agost 22, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments