SEKRETARIETI YA AJIRA YAWAFUNDA WANAFUNZI WALIOPO MASHULENI, YASEMA NI BUSARA KUOMBA USHAURI KABLA HUJAOMBA FANI KUJIUNGA CHUONI
Selemani Ahamadi
Daresalaam
Wanafunzi waliopo
mashuleni wameshauriwa kujiunga na kozi za masomo ya Afya,Elimu na Kilimo kama
kweli wanataka kuajiriwa moja kwa moja serikalini kwani kwa sasa sekta hiyo
kuna uhaba mkubwa sana wa wafanyakazi wake hapa nchini,
Akizungumza na
wanahabari hivi karibuni jijini Daresalaam ,Msemaji na mkuu wa kitengo cha
mawasiliano serikalini,ofisi ya rais sekretarieti ya ajira katika utumishi wa
umma Bi. Riziki Abraham amesema kwa sasa sekta ya afya,elimu na kilimo bado
zinamahitaji makubwa sana hivyo wanafunzi wanaootaka kujiunga na masongo ngazi
ya chuo ni vema wakajikita katika fani hizo ili kuondoa usumbufu wa kupata
ajira
WANAHABARI WAKIWA KAZINI,
Aidha Bi. Abraham
ameongeza kusema kuwa sekretarieti ya ajira wako katika mpango wa kuwawezesha
waombaji wa fursa za ajira kuwasilisha maombi yao ya kazi kwa mumo wa
kielektroniki (e-application) kwa nafasi wazi zitakazokuwa zikitangazwa katika
utumishi wa umma ili kurahisisha kupunguza mlolongo wa uendeshaji wa mchakato
wa ajira
Vilevile msemaji huyo
wa sekretarieti ya ajira amewataka wananchi kuondoa fikra potofu ya kuwa ni
lazima uwe na mtu wa karibu ili maombi yako yafanyiwe haki, kwani uendeshaji wa mchakato wa ajira katika
utumishi wa umma ni wa wazi na wa haki
HAPA AKIENDELEA KUTOA UFAFANUZI JUU YA MAWAZO POTOFU YALIJAA VICHWANI MWA WADAU KUWA NI LAZIMA UWE NA MTU WA KUKUBEBA ILI UPATE AJIRA,AMESEMA HAKUNA KITU HICHO |
“Nataka niwaambie
wanaomba fulsa ya kuajiriwa lazima wahakikishe wamefika viwango vinavyotakiwa
na nafasi inayoombwa vinginevyo huwezi kupata nafasi hiyo kwani vigezo na
mashariti lazima vifuatwe, hakuna kubebana katika mchakato mzima” Aliongeza Bi.
Abraham
Katika hatua nyingine
sekretarieti ya utumishi wa umma imetangaza idadi ya watu waliofoji vyeti
mbalimbali wakati wa kuomba nafasi wazi ya ajira na kwamba mpaka sasa jumla ya
vyeti 677 vya kughushi vimekamatwa ambapo wahusika wa vyeti hivyo wanadai
kuvipata katika taasisis za RITA,VETA na NECTA
Watu hao wameondolewa
katika mchakato na kwamba hatua za kisheria zitafuata ili kutoa funzo kwa
wengine wasiendelee na tabia kama hizo
No comments
Post a Comment