PINDA APOKEA SHEHENA YA KWANZA YA MABOMBA YA GESI,ASEMA SASA KAZI IMEANZA RASMI, ATAKA WADAU,WANAHARAKATI KUUNGA MKONO DHAMIRA YA SELIKARI
WAZIRI mkuu wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda amepokea shehena
ya kwanza ya mabomba ya kusafirishia gesi toka mkoa wa Mtwara hadi Kinyerezi
jijini Darealaam ujenzi utakaokamilika baada ya miezi kumi na minane
WAZIRI MKUU WA TZNANIA AKITOA NENO KWA WANANCHI WALIOHUDHULIA KATIKA MAPOKEZI YA SHEHENA YA KWANZA YA MABOMBA TOKA NCHINI CHINA,JUMLA YA MABOMBA 3500 YALIWASILI KATIKA BANDALI YA DARESALAA |
MABOMBA KABLA HAYAJASHUSHWA KATIKA MELI,MENGINE YAKIWA YAMESHIKWA NA FORKLIFT TAYARI KWA KUWEKA KATIKA MALOLI YALIOWEKA TAYARI KWA KUSAFIRISHA MABOMBA HAO KWENDA HUKO MTWARA |
MABOMBA YAKISHUSHWA TAYARI KWA SAFARI YA KWENDA MTWARA |
HAPA YAKIWA YAMESHAPAKIWA KATIKA GARI MAALUM TAYARI KWA SAFARI |
Akipokea shehena hiyo ya mabomba toka nchini China Pinda
amesema wadau wote kwa pamoja ni vema tukawa watoa elimu kwa wenzetu ambao kwa
namna moja ama nyingine bado hawana uwelewa mzuri wa umuhimu wa kusafirisha
gesi hiyo toka Mtwara kwenda Jijini Daresalaam
Pinda ameongeza kusema kuwa mradi huu unategemewa kuongeza
ajira kwa Watanzania na kwamba ukikamilika utatoa uhakika wa nishati ya umeme
na hivyo kuliondoa Taifa katika giza ambalo limekuwa likiisumbua taifa kwa muda
mrefu
Waziri wa nishati na madini Professa sospeter Muhongo Akifafanua jambo juu ya faida zitakazopatiakani pindi ujenzi wa mabomba hayo yatakapo kamilika |
Shehena hiyo imeingiza jumla ya mabomba elf tatu mia tano
(3500) ambayo yanaweza kujenga kilomita 40 toka mkoani Mtwara,
Naye mkurugenzi mtendaji wa TPDC akimkaribisha mgeni rasmi katika mapokei hayo
ya Mabomba ya kusafirisha gesi, amesema
huu ni mwanzo lakini zoezi kama hili litafuatia huko mkoani Mtwara
ambapo pia Waziri mkuu atakuwepo kupokea shehena hiyo ya pili hivi karibuni
MKURUGENZI MTENDAJI WA TPDC BW. YONNA KILLAGANE AKIFAFANUA JAMBO KATIKA MAPOKEZI YA SHEHENA YA KWANZA YA MABOMBA YA KUSAFIRISHA GESI TOKA MTWARA HA DSM |
Mradi huo wa kusafirisha gesi toka Mtwara utaighalimu
serikali jumla ya bilion 1.2 za marekani ambazo ni feha zetu tulizokopa toka
benki ya Exim ya China yenye riba nafuu, na hivyo kuondoa dhana iliyojengeka
kuwa mabomba haya ni ya watu wa china
No comments
Post a Comment