Zinazobamba

JESHI LA POLISI KANDA MAALUM YAWAKAMATA WEZI WA USIKU, NI MAJAMBAZI SUGU YANAYOTUMIA SILAHA ZA MOTO


,
Jeshi la polisi kanda maalum ya Daresalaam limefanikiwa kukamata silaha za moto saba na risasi kumi na tisa pamoja na mapanga ambayo yalitumika kufanya vitendo vya ujambazi katika mabweni ya Yombo one katika chuo kikuu cha Daresaalam

KAMISHINA WA POLISI SULEIMANI KOVA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI
Akizungumza na Blogu ya jamii ya FULLHABARI, DCP Ally Mlege kwa niaba ya Kamishina wa polisi kanda maalu ya Daresaalaam  Suleimani Kova, Mlege amesema  Mnamo tarehe 08-07-2013 huko maeneo ya ubungo katika kituo cha daladala jeshi hilo lilifanikiwa kuwakama  majambazi wanne wakiwa na silaha aina ya shorti gun ikiwa na risasi moja,lap top mbili aina ya Toshiba, simu aina ya sumsung model C3230

DCP Mlege ameendelea kubainisha kuwa majambazi hayo wamefanikiwa kuyakamata baada ya kuwawekea mtego kwa muda mrefu, watu hao maada ya mahojiano marefu wamekili kuhusika na uharifu uliotokea katika mabweni hayo june 21 saa tisa usiku  ambapo waliweza kumjeruhi mwanafynzi mmoja na kutokomea na mali za wanafunzi wa mabweni hayo

No comments