KUANZA KWA MSMU MPYA WA UNUZI WA NAFAKA,WAKULIMA WATAKIWA KUUZA MAZO YENYE UBORA WA HALI YA JUUU
Na selemani Magari
WAKALA wa hifadhi ya chakula (National food ResevesAgency)
imeanza mchakato wa kununua nafaka kwa wananchi na kuwatangazia wakulima wa
kanda saba za Kipawa,Arusha,Shinyanga,Dodoma,Makambako,songea na Songea
kupeleka bidhaa zake sokoni zikiwa na ubora unaotakiwa
MSEMAJI WA WIZARA YA KILIMO CHAKULA NA USHIRIKA bWANA RICHADI KASUGA AKIFAFANUA JAMBO MBELE YA WANAHABARI |
CHARLES WALWA, MKURUGENZI WAKALA WA TAIFA WA HIFADHI YA CHAKULA Bw. Charles Walwa akifafanua moja ya mswali ya wadau |
Akizungumza na wanahabari hivi karibuni, Mkurugenzi wa
wakala wa taifa wa hifadhi ya chakula Bw. Charles Walwa amesema kuwa kwa sasa
tathimini fupi iliyofanywa na wizara inaonyesha kuwa hali ya chakula kwa mikoa
yote 25 ni nzuri na kwamba wao wataanza mchakato wa kununua nafaka katika
maeneo ambayo kuna dhiada
Ameendelea kusema kuwa katika mwaka huu jumla ya vituo 58
vitatumka katika ununuzi wa nafaka, hivyo wananchi wanashauriwa kupeleka nafaka
zao katika vituo hivyo,pia ametoa angalizo kwa wananchi kupeleka nafaka kwa
wakala ambazo tu zimekidhi vigezo
Naye mkurugenzi msaidi wa utafiti wa mazao Bw. Hussein
A.Mansoor ameongeza kusema kuwa kwa sasa kumebainika ugonjwa hatari wa mahindi
uitwao maize lethal necrotic (MLND) ambao umeanzia huko nchi za jirani za Kenya
na kwamba tayari serikali imeshachukua tahadhari zote za kuondoa ugonjwa huo
kuingia nchini,amesema ugonjwa huo kwwa sasa hauna tiba
No comments
Post a Comment