NBC YAZINDUA KAMPENI YA MIKOPO KWA WAFANYA KAZI WAAJIRIWA
Benki ya taifa ya Biashara NBC Imezindua kampeni ya uelewa
ya mikopo kwa makundi, ambapo kupitia kampeni hiyo mteja anayehitaji kukopa
benki hiyo ni lazima awe muajiriwa na
kwamba sharti pekee la kukubalka ni uthibisho wa barua ya muajiri wako na sio
vinginevyo
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo makao makuu
ya benki hiyo jijini Daresalaam Mkurugenzi mtendaji wa benki hiyo Bi.Mizinga
Melu amesema uzinduzi huo umekuja wakati muafaka kwa waajiiriwa ambao walikuwa
hawapati fulsa za kuomba mikopo kwa kukosa sifa zinginezo katika benki hiyo
sasa wanaweza kuomba mikopo kupia sifa za kuajiriwa,
Benki ya biashara ya Taifa inauzoefu wa kufanya huduma za
kipesa hapa nchini kwa takribani miaka 45 na kwamba ina matawi zaidi ya 52 na
ATM ZA VISA zisizopungua 280 nchini kote hivyo ni vema watumishi wakachangamkia
mikopo hiyo
No comments
Post a Comment