TOENI TAARIFA ZA UJANGIRI, ATAKA WANANCHI KUJUA FISI NAO NI HATARI
Wananchi wametakiwa kutoa ushirikiano katika vita dhidi ya
ujangiri kwani kufanya hivyo kutasaidia kwa kiasi kikubwa kupambana na ujangiri
ambao unaendelea kwa kasi
| KAIMU MKURUGENZI MSAIDIZI, UZUIAJI UJANGIRI Bw. John Muya.akifafanua jambo kwa waandishi wa habari juu ya umuhimu wa kushirikiana kuchunga rasilimali zetu za asili |
Akizungumza na wanahabari jijini Daresalaam hivi karibuni,
Mkurugenzi mtendaji wa idara ya wanyama pori,Bw.
Alexanda Songorwa amesema dhima ya kulinda rasilimali ya taifa hili ni la kila
mmoja na kwamba wananchi waondokane na fikira potofu ya kudhani jukumu la
kulinda rasilimali zetu ni za wizara ama maafisa wanyama pori
| Hapa mkurugenzi idara ya wanyama poli Alexanda Songorwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya dhima ya kushirikiana katika utoaji taarifa kwa ujangiri wowote utakaojitokeza |
No comments
Post a Comment