Zinazobamba

TANZANIA KUUZA UMEME NJE MWAKA 2014


Tanzania sasa itakuwa na uwezo wa kuuza umeme wake nje ya nchi ifikapo mwaka 2014 baada  ya TANESCO kutiliana saini mkataba  na kampuni ya china ya kuzalisha umeme wa gesi ya mtwara.

Akizungumza katika sherehe ya kutiliana saini ya mkataba huo waziri wa nishati na madini Sospeter Muhongo alisema kuwa kituo hicho cha uzalishaji umeme wa gesi kitajengwa katika eneo la kinyerezi jijini Dar es salaam na inatarajiwa kumalizika mwaka 2014

Waziri Muhongo aliongeza kuwa mradi huo utaweza kuzalisha megawati 600 na  unatarajiwa kugharimu kiasi cha dola milioni 300 za kimarekeni

“Mradi huu ukikamilika utasaidia kuboresha uchumi wa nchi kuongeza pato la taifa , tutaboresha barabara,shule na hospital hapa nchini” aliongeza Waziri.

BALOZI WA CHINA HAPA NCHINI LUI ZOGHUO AKIZUNGUMZA KATIKA SHUGHULI HIYO

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI MH.SOSPETER MUHONGO,MKURUGENZI WA TANESCO MH.FELCHEMI MRAMBA WAKIMSIKILIZA KWA MAKINI BALOZI WA CHINA HAPA NCHINI

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI SOSPETER MUHONGO AKIZUNGUMZA KATIKA SHUGHULI HIYO

No comments