Zinazobamba

DC KINGALAME AIPONGEZA TBA KWA MRADI WA MAKAZI YA BIASHARA MKOANI GEITA.


Na Richard Mrusha 

Mkuu wa Wilaya ya Nyan'gware Grace Kingalame ameipongeza wakala wa Majengo Nchini( TBA) kwa kuja na wazo la kuanzisha mradi mkubwa wa makazi ya biashara Mkoani Geita kwani itasaidia Wananchi kupata makazi bora kwa gharama nafuu.

DC Kangalame  ametoa pongezi hizo Septemba 24,2025,alipofanya ziara ya kutembelea maonesho ya nane  ya teknolojia ya madini yanayofanyika katika viwanja vya Dkt.Samia Suluhu Hassan Bombambili Mkoani Geita.

Aidha amesema TBA imefanya vizuri kubuni  wazo la kuanzisha mradi mkubwa wa makazi ya Biashara Mkoani humo jambo ambalo linachochea upatikanaji wa makazi bora hivyo,nakuomba iendelee kufanya kazi hiyo nzuri katika maeneo mengine.

Ameongeza kuwa mradi wa makazi ya biashara ni wazo ambalo linaendelea kutafsiri maono na matazamio ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha watanzania wanapata makazi bora.Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Wilaya ya Nyang'wale ameipongeza TBA kwa uamuzi wa kushirikiana na sekta binafsi  kuendeleza Miradi mikubwa Nchini.

 "Natumia,nafasi hii kuitaka sekta binafsi ichangamkie fursa hii ya kushirikiana na TBA ili makazi hayo yakamilike kwa muda muafaka ".amesema DC. Kingalame

Nakuomgeza kuwa "Makazi haya yataleta raha kwa sababu watumishi na wananchi kwa ujumla watapata Makazi bora ya kuishi".

Aidha amesema kuwa tafsiri ya Rais Dkt.Samia ni kuona Wananchi wake wanaishi kwenye maeneo mazuri,hivyo mradi huo utakua sehemu ya maono ya mheshimiwa Rais. 

No comments