DC KANGALAME AIHAKIKISHIA BOT KUENDELEA KUPATA DHAHABU MKOANI GEITA.
Na Richard Mrusha
Mkuu wa Wilaya ya Nyan'gware Grace Kingalame mesema kwamba watu wanaendelea kuleta dhahabu ambayo BOT inainunua.
Amesema kuwa hadi sasa wanayo akiba ya dhahabu takribani tani 10.
DC Kingalame amesema BOT imepiga hatua kubwa katika eneo hilo nakwamba Serikali Mkoani Geita itaendelea kuweka Mazingira mazuri ya uwekezaji ili dhahabu ipatikane kwa wingi na BOT iendelee kuinunua.
"Nijambo la msingi kumpongeza rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa Tanzania kuwa miongoni mwa nchi tano zinazozalisha dhahabu kwa wingi barani Afrika na hivyo kuwa na akiba ya dhahabu ya kutosha"amesema
Amesema hayo septemba 24,2025 wakati wa ziara ya kutembelea maonesho ya nane ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika Katika viwanja vya Dkt.Samia Suluhu Hassan Mkononi GeitAmewasihi wachimbaji hususani wa Nyang'wale kuendelea kuiuzia Serikali na nje ya mipaka ya Tanzania kwa sababu Serikali haijawabana na imeweka mazingira mazuri ya kila mtu aweze kufaidika lakini nchi pia iweze kubaki na akiba ya dhahabu.
Ametumia fursa hiyo kuwaasa wananchi kutoka katika maeneo mbalimbali kufika katika viwanja hivyo ili wajifunze teknolojia inavyozidi kukua ya dhahabu kwa maana ya uchimbaji, uchenjuaji na uchorongaji.
DC Kingalame amefurahishwa na mabanda mbali ambapo amejionea teknolojia inavyozidi kusonga mbele.
Pia amefurahishwa na wajasiriamali wanavyojishughulisha na kujipambanua katika suala zima la utafutaji fedha na kukuza uchumi wao na Taifa kwa ujumla.
No comments
Post a Comment