Zinazobamba

MOI YAJA NA HUDUMA YA KUWEKA MIADI

Na Richard Mrusha 

Wananchi wameaswa kutumia huduma ya kuweka miadi kupitia njia ya mtandao ili kupunguza msongamano wa wagonjwa wanaotokea nje ya mkoa wa Dar Es Salaam na hivyo kuwapunguzia muda mrefu wa kusubiri kupata huduma.

Daktari wa mifupa kutoka Taasisi ya Mifupa na Ubongo (MOI) Kenneth Mngidange amezun.gumza na waandishi wa habari Sept 24,2025 kwenye maonesho ya Nane ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika Katika viwanja vya Samia Suluhu Hasan mkononi Geita.Amesema Huduma zinazotolewa MOI ni pamoja na upasuaji wa ubongo,kutoa uvimbe kupitia uvungu au sakafu ya pua,upasuaji wa mgongo kupitia matundu na Teknolojia unde (AI) ,Upasuaji magoti kupitia matundu.

Amesema MOI inatoa huduma nyingi za kibobezi ambazo wananchi wa Geita wanaweza kunufaika nazo.

Ameongeza  kuwa  tangu wafike kwenye maonesho hayo wananchi zaidi ya 170 wamejitokeza na kupata ushauri wa matibabu na baadhi ya wananchi wameshauriwa kwenda hospitali za karibu kufanya vipimo zaidi.

No comments