Home
/
Unlabelled
/
KILOSA YAZIZIMA MAPOKEZI YA MGOMBEA URAIS AAFP,AWAAHIDI MAKUBWA,VIWANDA VYA SUKARI KUJENGWA.
KILOSA YAZIZIMA MAPOKEZI YA MGOMBEA URAIS AAFP,AWAAHIDI MAKUBWA,VIWANDA VYA SUKARI KUJENGWA.
*Polisi kuishi kifalme.
*Maprofesa ubunge ni ndoto tena.
*Wachungaji marufuku kuingia kwenye siasa
Na Mwandishi Wetu.Kilombero.
Wananchi wa Kilombero wameahidiwa kuongezewa Viwanda kwa ajili ya uzalishaji wa Sukari kwani Viwanda vilivyopo kw sasa vinamnyanyasa mkulima na kusababisha bei ya Sukari kuwa juu.
Ahadi hiyo imetolewa Septemba 5 2025 katika la Kilombero K2 Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro na Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Wakulima AAFP Kunje Ngombale Mwiru wakati akihotubia mamia ya Wananchi waliojitokeza kumlaki.
"Ndugu zangu Watanzania kumbe tunalalamika Sukari inauzwa bei kubwa kumbe,wakulima wananyanyasika,wakilima miwa wananyayaswa na wenye Viwanda,watu wanabadilisha mashamba ya miwa sasa hivi wanalima mpunga,halafu kumbe ndio maana wanataka Sukari iagizwe nje ili mafisadi waweze kufisadi zaidi,Serikali yangu haiwezi kukubaliana na hilo kabisa,"amesema.
Nakuongeza kuwa " Nilidhani kwamba huku Kilimo kinaendelea na Wakulima wananufaika kwenye chama chao ushirika,nimeambiwa kuna mua wa ndani na mua wa nje,nilimuliza Mzee wangu mua wa ndani na mua wa nje maana yake ni nini?..kumbe nika gundua mua wa ndani niwa mwenye kiwanda,na mua wa nje niwa malala hoi(mkulima),chagueni chama chenu cha AAFP vyama vyote vya ushirika navifuta.
*Polisi kuishi kifalme.
Aidha amesema kuwa askari polisi wamekua wakifanya kazi kubwa ya kupambana na wahalifu na kuhakikisha Watanzania wanaishi kwa amani na mali zao lakini mishahara yao ni midogo,hivyo Serikali yake itakapoingia madarakani itabirsha mslahi ya polisi.
"Hawa polisi unaowaona hapa wanafanya kazi kubwa ya kupambana na wahalifu,hawa ni Wazalendo wakubwa lakini ukifuatilia mishahara yao ni midogo sana,hivi mnavyowaona hapa tangu sisi tumetangaza tunakuja sidhani hata chai kama wamekunywa kwa hali hii ya kulinda usalama wenu,Serikali yangu nikingia madarakani polisi wataishi kifalme."amesema Mheshimiwa Mwiru.
*Maprofesa Ubunge kwaheri.
Aidha amesema kuwa Serikali inatumia fedha nyingi kusomesha Watanzania hadi wanakua maprofesa lakini wamekua wakiacha kazi walizosomea nakuingia kwenye siasa,hivyo Serikali yake haitokubaliana na hali hiyo.
"Serikali inasomesha kwa fedha kubwa mtu anakua profesa,leo Profesa huyu amejifunza mambo mengi amejifunza mambo ya Madini,Miamba,kufuga nyuki,Kilimo,lakini anaacha fani yake ambayo Serikali imemlipia gharama kubwa,fedha ambazo zingesaidia kujenga Zahanati lakini akienda huko u
akirudi anakuja kuomba ubunge anaachana na fani yake,Serikali yangu hakuna Profesa atakaekua Mbunge,Profesa kazi yake nikufundisha Watanzania hawa ambao wanahamu yakujua ujuzi wa aina mbalimbali.
*Marufuku Mchungaji kujiingiza kwenye siasa.
Mheshimiwa Mwiru pia amesema kuwa Serikali yake endapo atashika dola haitoruhusu wachungaji wa dini kuingia katika masuala ya siasa kwani wao wana maono yao na wana aminiwa na watu kulingana na maoni yao,hivyo kujiingiza kwenye siasa ni uvunjifu wa amani.
"Serikali yangu haitakua inachanganya changanya watu,hilo jambo halipo,Serikali iliyopo sasahivi madarakani imewachukua wachungaji badala ya kuhubiri amani wamewaleta kwenye ubunge,kwenye Serikali,Serikali yangu haitokubaliana na hilo,mchungaji atabaki kua na uchungaji wake,hakuna haja yakuwapokea watu wanaoitwa wachungaji kwasababu wana maono yao,na watu wana waamini kwa maono yao,sasa leo unamkaribisha kwenye siasa analeta maono kwenye siasa hilo halotowezekana.
Pia mgombea urais huyo wa AAFP amesisitiza kabla ya kuingia Ikulu atahakikisha linajengwa bwawa la mamba kwa ajili ya kuwashughulikia Mafisadi wanaotafuna fedha za wanyonge.
"Siwezi kwenda Ikulu nikawaamcha mafisadi nje wakitembea na vitambi,nitasubiri mpaka bwawa la mamba lichimbwe ndani ya Ikulu nami ndo nitaenda nitaongea na idara ya usalama wa Taifa, haiwezekani nimetangazwa leo kua rais kesho nikimbilie kwenda Ikulu halafu mafisadi nawaacha nje wanaendelea kuwanyonya Wananchi.
*Asisitiza Uzalendo.
"Kama inavyosema Ilani yetu na sera zetu,vipaumbele vyetu vya kwanza kabisa ni uzalendo kwenye Bunge, uzalendo kwenye Mahakama, na uzalendo kwenye Serikali,changamoto zote zinatokana kwasababu ya watu kukosa uzalendo."
Aidha amesema, Watanzania wanapoelekea wanaendelea kukosa uzalendo,ndio maana ameamua Serikali yake kua ya mchakamchaka kwamba kazi itafanyika kwa masaa 24,ili kuweza kupata maendeleo ya kweli kwani kila kukicha ni vilio Wananchi wanahitaji mabadiliko.
"Ndugu zangu wana Kilosa safari hii ya mabadiliko siyahiali, niya lazima ili tuweze kufanya mabadiliko ya kweli,kila ninapopita changamoto ninazikuta Watanzania waliowengi wanakosa uzalendo,nimeona kutoka Mikumi kuja hapa mkandarasi alijenga barabara lakini imekua nyembamba nikiwa rais tutavunja mawe na kujenga barabara. "
KILOSA YAZIZIMA MAPOKEZI YA MGOMBEA URAIS AAFP,AWAAHIDI MAKUBWA,VIWANDA VYA SUKARI KUJENGWA.
Reviewed by mashala
on
13:19:00
Rating: 5

No comments
Post a Comment