TAARIFA YA KUPOTEA KWA ALIYEKUWA MSAIDIZI WA POLEPOLE
Kumekuwa na taarifa ya kupotea kwa Ndg Pius Mpweza (Aliyekuwa Msaidizi wa Hamphrey Polepole) ikielezwa na Suzan Mpweza ambaye ni Dada wa Pius, mkazi wa Kigamboni, Vijibweni Dar es Salaam.
Suzan amejitokeza jioni ya leo Ijumaa September 5 akieleza namna ambavyo amemtafuta Kaka yake kwa muda mrefu bila mafanikio
Suzan anaeleza -"Leo asubuhi hakuonekana kazini kwake kama ilivyo kawaida yake na alipotafutwa, simu zake zilikuwa zimezimwa"
"Awali kabla ya kumaliza kazi zake jana jioni, Ndugu Pius alisema kwamba alitarajia kuzungumza na waandishi wa habari kwa mara ya pili leo mchana, kuhusu kauli mbalimbali ambazo zimekuwa zikitolewa na Ndugu Polepole."
"Pia Ndugu Pius, alilalamika kuwa Ndugu Polepole amekuwa akimpigia simu mara kwa mara lakini hakutaka kuzipokea."
"Baada ya kuona hampati, Ndugu Polepole alituma watu kumpigia simu Ndugu Pius kumuonya aache kumzungumzia na baadae, Ndugu Polepole alimwandikia Ndugu Pius ujumbe wa maneno akimuonya kuacha kuzungumza kuhusu yeye, lasivyo angeweza kumpoteza mjini."
"Ndugu Pius alitoa taarifa ofisini kwake pamoja na kwenye familia kuhusu ujumbe huo ambao umehifadhiwa kwa hatua zaidi na kueleza akipotea, wa kuulizwa ni Ndugu Polepole."
"Wenzake walipoona hajafika eneo la kazi kama ilivyo kawaida na simu zake hazipatikani na kwa kuzingatia kwamba aliripoti kuhusu kutishiwa na Ndugu Polepole, waliamua kuja kuulizia nyumbani ."
"Walipofika nyumbani niliwapokea nikaulizwa kuhusu Pius , nikiwajibu kuwa toka jana usiku hajarud nyumban labda amepata safari."
"Kutokana na vitisho hivyo na ukweli kuwa Ndugu Pius hapatikani sisi ndugu zake, tunamtaka Ndugu Polepole atoke hadharani kueleza alipo Ndugu yetu Pius."
"Ndugu Polepole asipotoka kueleza ndani ya saa 24 alipo Ndugu yetu Pius, tutaweka hadharani meseji ya Ndugu Polepole na sauti za watu waliotumwa na Ndugu Polepole kumpigia Ndugu Pius ambazo zimerekodiwa."
No comments
Post a Comment