AAFP KUWAPA KIPAUMBELE WAKULIMA NA WAFUGAJI.
*Yaahidi kuwanyonga Mafisadi na kuwaondolea nguvu za kiume wabakaji.
Na Mussa Augustine.Kisaki Morogoro.
Ameyasema hayo leo August 31,2025 katika kata ya Kisaki Wilaya ya Morogoro Mkoani Morogoro wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi,nakubainisha kuwa atahakikisha Serikali yake inatembea sambamba na makundi hayo muhimu ili kuyainua kiuchumi.

"Asilimia kubwa ya Watanzania wanazalisha chakula,hivyo Serikali yangu itaweka maeneo stahiki ili kuondoa migogoro kati ya Wakulima na wafugaji,".amesema kunje wakati akiwahotubia Wananchi wa kata ya Kisaki.
Pia amesema kwamba Viongozi na Wananchi wanapswa kuwa Wazalendo ili Taifa lisiweze kuyumba na kukosekana kwa amani na utulivu,ambapo ni tunu zilizoachwa na waasisi wa Taifa la Tanzania.
"Nchi yetu haina Wazalendo,hata kama tukileta malaika kutoka mbinguni kama hakuna uzalendo Taifa litayumba" amesema Mwiru.
Nakuongeza kuwa"Chama hiki(AAFP) nichakwenu nyinyi wakulima,muwe makini wasije watu wenye sera za uongo wakawarubuni,nichagueni mimi Kunje Ngombale Mwiru kuwa rais wenu,pamoja na Mgombea mwenza wangu Chumu Abdallah Juma pamoja na Mbunge,na diwani katika kata hii ya Kisaki".
Hata hivyo amebainisha kuwa Serikali yake itafungua madawati ya kufundisha uzalendo nakwamba kazi hiyo itafanywa na wastaafu ambao wameitumikia Serikali yao.
Sambamba na hilo amesema kuwa endapo atapewa ridhaa yakua rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atahakikisha anawachukulia hatua kali mafisadi ikiwemo kuwanyonga hadi kufa kwasababu wanajimilikisha mali za wanyonge.
Chumu Abdallah JumaNae Mgombea Mwenza Chumu Abdallah Juma ameonesha kusikitishwa na vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia nakuahidi kuvishughulikia pindi Wananchi watakapo kichagua chama Cha AAFP kushika dola siku ya uchaguzi Mkuu Oktoba 29,2025.
Katibu Mkuu AAFP Rashid RaiAwali Katibu Mkuu AAFP Taifa, Rashid Rai amesema kuwa kata ya Kisaki ni kata yenye heshima kwa chama chao kwani chama hicho kiliasisiwa kwenye kata hiyo,nakuongeza kuwa kina mpango wa kuwatetea wakulima ambao wanaonekana wanyonge na kudhalilika.
Amesema kuwa AAFP ikishika dola huduma za afya pamoja na Elimu zitatolewa bure,kwani Tanzania ni nchi tajiri kutokana nakuwepo kwa rasilimali nyingi ambazo Wananchi hawanufaiki nazo.
Amesema pia kuwa Serikali ya AAFP itahakikisha inafuta vyeo vyote vya ukuu wa Mkoa,Wilaya pamoja na ukatibu tawala nchi nzima,nakufanya kuwa na Serikali ndogo inayofanya kazi zaidi kupitia kauli mbiu ya " maendeleo ni lazima"
Nao wagombea Ubunge kupitia Chama hicho na Majimbo yao kwenye mabano akiwemo Yusuph Rai(Temeke) Ndonge Said Ndonge( Mbagala) pamoja na Shani Ally Kitumbua(Chamazi) Dar es salaam na Mgombea udiwani kata ya Kisaki Wilayani Morogoro Ally Mshamu Mtawila"chachala" wamesema kwa nyakati tofauti kuwa chama hicho kikishika dola kitashughulikia kero zote zinazowakabili wananchi katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya Afya,Elimu na miundombinu ya barabara na Maji.
Yusuph Rai Shani Ally Kitumbua Mgombea udiwani Ally Mtawila
No comments
Post a Comment