Zinazobamba

MGOMBEA UBUNGE AAFP JIMBO LA MOROGORO KUSINI AJITOA KWENYE KINYANG'ANYIRO.


Takukuru yaombwa kufanya uchunguzi haraka.

Kunje,Rai walia na rafu za CCM,waitaka iache mara moja.

Na Mwandishi Wetu.

Chama Cha Wakulima (AAFP)kimeitaka Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi(INEC) kufanya uchaguzi wa marudio katika maeneo yote nchini ambayo amebaki Mgombea mmoja pekee wa CCM. 

Hatua hiyo imekuja baada ya Mgombea Ubunge Jimbo la Morogoro Kusini kupitia Chama Cha Wakulima (AAFP)Uwesu Bakari Ally Nyalupara kuwasilisha brua ya kujiondoa katika kinyang'anyiro cha kugombea ubunge katika Mazingira ya kutatanisha.

Rai hiyo imetolewa leo Septemba 1,2025 na Mgombea urais kupitia Chama Cha Wakulima(AAFP) Kunje Ngombale Mwiru wakati akihotubia Wananchi wa Kata ya Mvuha Wilaya ya Morogoro nakusema kuwa endapo kutakua na Kiongozi wa CCM amehusika kumshawishi Mgombea huyo ili ajitoe kwenye uchaguzi achukuliwe hatua kali za kisheria.

" Mimi nitakua Mgombea wa kwanza kujiondoa kati ya wagombea 16 tuliobaki,endapo hatua zozote hazitachukuliwa kwa Mtu aliyehusika kumrubuni Mgombea wetu ili awasilishe  barua ya kutoshiriki kwenye uchaguzi mkuu"amesema Kunje.
Nae Katibu Mkuu wa Chama hicho Rashid Rai ameitaka TAKUKURU kuchungza kwa haraka viashiria vya rushwa kwa Mgombea huyo aliyejiuzulu nakuwataka pia viongozi wa CCM kuacha tabia ya kuwashawishi wagombea wa vyama pinzani ili wasishiriki kwenye uchaguzi kwani kufanya hivyo ni aibu kwa Taifa.

"Naomba TAKUKURU ifanye uchuguzi haraka kuhusiana na kitendo hiki,haiwezekani Mgombea wetu ajiondoe dakika za mwisho,kuna kitu nyuma ya pazia,kuna viashiria vya rushwa " amesema Rai.
Nakuongeza kuwa" Tume huru ya uchaguzi ihakikishe uchaguzi unarudiwa kwenye maeneo ambayo anaonekana kuna Mgombea mmoja tu wa CCM,ikitokea hivo lazima uchaguzi mdogo uitishwe kwasababu wagombea wengi wanajitoa kwasababu ya kushinikizwa kwa vitisho pamoja na fedha. 




No comments