Home
/
Unlabelled
/
AAFP MOROGORO NI MOTO,YADAI MEMORI YA CCM IMEJAA,WANANCHI KUIPUMZISHA OKTOBA 29 MWAKA HUU.
AAFP MOROGORO NI MOTO,YADAI MEMORI YA CCM IMEJAA,WANANCHI KUIPUMZISHA OKTOBA 29 MWAKA HUU.
Na Mussa Augustine:Morogoro.
Yusuph Rai ambae pia ni Mgombea Ubunge kupitia AAFP Jimbo la Temeke Mkoani Dar es salaam amesema hayo Septemba 4,2025 mjini Morogoro wakati akizungumza na Wananchi katika Viwanja vya soko la Mawenzi ikiwa ni muendelezo wa kampeni za uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 29 Mwaka huu.
Amesema kuwa Serikali ya AAFP imejinasibu kuleta maendeleo kwa kuanzia pembezonj mwa miji ili kuleta mjini,kwani Wananchi waishio pembezoni wamesahaurika kimaendeleo.
"Mjini tayari wenzetu waliotangulia wamefanya maendeleo mbalimbali ambayo yanaonekana,sasa sisi tunasema hivi wao wamefanya kwa kiasi chao lakini walipoishia tusiwalaumu."amesmea Yusuph
Nakuongeza kuwa"Yaani leo tukisema CCM haifai tutakua tunakosea sana,tuseme tu kwamba CCM memori yao imejaa, kwasababu yapo waliyoyafanya mazuri,yapo waliyoyafanya mabaya,lakini yale mazuri waliyoyafanya tunashukuru,na yale mabaya tunahitaji tuyaboreshe kupitia kwa Serikali.
Aidha amewaomba Wananchi wakichague chama hicho ili kiweze kutetea katika mambo mbalimbali hasa masuala yanayogusa watu,kwani chama hicho kinafanya siasa na maisha ya watu kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 9 ambayo inasema utajiri wa nchi hii utatiliwa maanani katika jitihada za kuondoa umasikini,ujinga na maladhi.
"Madhumuni makubwa ya chama chetu tunafikiria yakwamba,mkitupa Serikali tutaitumia ibara ya 9 ya katiba kwenda kuondoa mambo makubwa matatu ambayo ni umasikini,ujinga na maladhi".
Aidha amesema kuwa amewahi kutembelea magereza ya Keko,Ukonga pamoja na Segerea nakubainisha kuwa sehemu kubwa ya wafungwa waliomo gerezani ni Vijana kwasabubu wamekata tamaa na Taifa lao,hivyo Ilani ya AAFP itazingatia zaidi masuala ya ajira na afya kwa Vijana.
AAFP MOROGORO NI MOTO,YADAI MEMORI YA CCM IMEJAA,WANANCHI KUIPUMZISHA OKTOBA 29 MWAKA HUU.
Reviewed by mashala
on
13:37:00
Rating: 5

No comments
Post a Comment