Zinazobamba

AAFP YAAHIDI BOMBA LA MAJI KILA NYUMBA KILOSA.


Na Mwandishi Wetu.

Chama Cha Wakulima (AAFP) kimesema kinahitaji viongozi watakaosimamia Uzalendo na kufanya kazi ambayo watakua wametumwa na Wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hayo yamebainishwa Septemba 5 ,2025  na Mwenyekiti wa baraza la Vijana Taifa Yusuph Rai wakati akimnadi Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama hicho Kunje Ngombale Mwiru,katika Viwanja vya Kilombero K2 Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro.

"Sisi tunasema tunataka ustawi wa maendeleo ya Wananchi na sio kuja kushindanisha vyama vya siasa,vyama ni sehemu tu ya kisehemu kidogo sana lakini tunahitaji watu watakaosimamia uzalendo,watakaofanya kazi ambayo watakua wametumwa na Wananchi  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania sio chama chake."amesema Yusuph Rai,ambaye pia ni Mgombea Ubunge Jimbo la Temeke Mkoani Dar es salaamNakuongeza kuwa"sisi hatujaja hapa kushindanisha vyama, tukishindanisha vyama,sisi chama chetu bado ni kidogo mno sisi tumewaletea jembe Kunje Ngombale Mwiru ambaye tunaamini kwa wagombea wote 17 wa urais,tunaamini huyu anatosha,kwasababu kwanza ni kijana ambeye anaweza kutembea mchakamchaka kufika kwenye maeneo husika ambayo yana shida na akatoa maamuzi papohapo shida hiyo ikatatuliwa,

tumetengeneza kitu kinaitwa Ilani tumemkabidhi Mheshimiwa,Ilani tuliyotengeneza tulichukua muda mrefu sana na mimi nilikua katika hiyo timu ya uandaaji wa Ilani,tulisema tunataka tutengeneze Ilani itakayowagusa watu,hatutaki tutengeneze Ilani ya kuchekesha, sisi sio chama cha kuchekesha eti tuje tuwaambie Watanzania wana shida ya ubwabwa sisi hatuna mambo hayo".amesemaAidha amesema kuwa chama hicho kimeenda kuwambia Wananchi kuwa Watanzania wanashida ya hospitali, Walimu,pia shida ya upatikanaji wa haki,na shida ya upatikanaji wa maji safi na salama.

"Wenzetu wanajinasibu kwamba wameweka kampeni nchi nzima ya kumuondoa mama ndoo kichwani lakini bado Wananchi wanaenda kuteka maji katika maeneo tofauti tofauti."amesema Yusuph 

Nakuongeza kwamba"Maana ya kumtua  ndoo mama kichwani,ni  kila nyumba kunakua na bomba la kupata Maji safi na salama kwa saa 24, mkichagua chama hiki kwenye Ilani ya chama chetu tumesema yakwamba tutatengeneza gridi ya Taifa ya Maji, ambayo yatasambazwa kila kaya kama ulivyosanbazwa umeme,hii ndo tafsiri sahihi ya kumtua ndoo mama kichwani." amesema.






No comments