Zinazobamba

AAFP KUWAONDOA NGUVU ZA KIUME WABAKAJI NA WALAWITI.


Na Mwandishi Wetu.Kilosa.

Chama Cha Wakulima (AAFP)kimesema kuwa endapo kitashika dola kitahakikisha kinamuondoa nguvu za kiume mwanaume yeyote atakaekamatwa na kosa la kubaka na kulawiti na ushahidi ukiwa wa uhaka hali itasaidia kumfanya asibake tena mtu mwingine.

Kauli hiyo imetolewa Septemba 5,2025 na Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake AAFP Taifa Shani Kitumbua wakati akizungumza na Wananchi wa Kilombero K2 Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro kwenye kampeni za kumnadi Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama hicho.

"Ndugu zangu tunajua sasahivi hali ya hewa imebadilika,Wazazi wenzangu leo hii watoto wa kiume wanalindwa kuliko mtoto wa kike,watoto wa kiume ushoga umejaa sana,mlinde sana mtoto wako wa kiume usiwe bize na kulima,wala kitu kingine,watoto wanatekwa na wanaowateka wanaondoka nao sijui wanawapeleka wapi!"ameongea kwa kusikitika Kitumbua.Kitumbua ambaye pia ni Mgombea Ubunge Jimbo la Chamazi Mkoani Dar es salaam,ameongeza kuwa" sisi kama Serikali ya AAFP tunataka kwamba mtu yeyote atakae kamatwa na kosa la kubaka au kulawiti tunamtoa nguvu za kiume kwasababu akishafungwa miaka thelathini tunawajaza wangapi,na wakienda huko magereza wanaenda kubakana tena hakuna mtu atakaeshughulikia, kwahiyo tumemuongezea wasifu(CV) mbakaji aende akabakane tena,hicho kitu hatutaki.

Akizungumzia changamoto zizaowakabili Wananchi wa Kilombero K2 na maeneo mengine wilayani Kilosa Bi.Kitumbua amesema kuwa wananchi hao wanakumbwa na matatizo mbalimbali ikiwemo  katika sekta ya Kilimo pamoja na Afya licha ya Serikali ya CCM kujinasibu kuwa imefanya maendeleo Makubwa.

"Tunajua shida zipo nyingi sana,CCM na Serikali yake imetutesa sana, tumeambiwa hapa Kilombero kuna kero nyingi sana hadi watu wamenyang'anywa mashamba ya miwa, mtu anaanza kulima akiwa na umri wa miaka ishirini tu leo ana miaka sitinj ananyang'anywa shamba lake la miwa, mtu huyu anaishije!"Nakuongeza kwamba "kweli Serikali imejaa ubabaifu mkubwa,naomba tubadilike kama ninavyosema mabadiliko ni lazima,kama ni mwana CCM baki na CCM yako lakini badilika chagua kiongozi aliye sahihi.".

Kuhusu huduma za afya Kitumbua amewambia Wananchi kuwa suala la huduma ya Afya limekua likisumbua wanachama,ambapo mtu akiumwa akienda hospitali hakuna dawa za kumtibu,huku maiti zikizuiliwa kuchukuliwa na wapendwa wao kutokana na kudaiwa,hali ambayo amesema ni fedheha na aibu kubwa kwa Taifa kudai maiti.

" Tunataka Serikali yetu ya AAFP kila kitu kitakua bure,hata kama kutakua na malipo basi yatakua ni malipo madogo mno,hasa upande wa maiti nikuidhalilisha maiti,huwezi kuiacha maiti mwezi mzima mtu unamdai milioni kumi kama alishindwa laki mbili ya kulipia dawa leo maiti anakuja kudaiwa milioni kumi ili iwe nini"?amehoji KitumbuaKatika hatua nyingine amewaasa Vijana kutokukubali kuandamana kwani wao ndio watakaoumia na familia zao,huku wale waliowahamasisha kuandamana wakiwa salama na familia zao. 

"Vijana achaneni na habari za kuandamana, wewe utaumia familia yako ndo itateseka,mbona wanaohamasisha muandamane hawaleti familia zao mbele!,mbona familia zao hazijawahi kuumia?,lakini nyinyi watoto wa masikini ndio mnaokaa mnaumia kila siku, kuandamana sio suluhu ya tatizo" amesema Kitumbua. 





No comments