RAI ACHUKIZWA NA UGATUZI WA MADARAKA.
*Asema viongozi wengi Serikali ya CCM wamekua wakimsifia rais huku wakisahau kuwatumikia wananchi.
*Asisitiza AAFP kuwafuta Wakuu wa Mkoa,Wilaya na Makatibu tarafa nchi nzima.
Na Mwandishi Wetu.Kilombero
Katibu Mkuu wa chana Cha Wakulima (AAFP)Rashid Rai amesema kuwa mfumo wa ugatuzi wa madaraka uliopo kwa sasa umebomolewa ndio maana viongozi wengi wameshindwa kuwatumikia wananchi na badala yake kumtukuza kiongozi wao wa juu ambaye ni rais.
Amesema hayo Septemba 5 ,2025 Kilombero Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro wakati akimnadi Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Wakulima AAFP Kunje Ngombale Mwiru,nakusema kuwa Serikali ya AAFP inataka kutengeneza Serikali ambayo Kila Mamlaka iloyotajwa kwa mujibu katiba na sheria iwajibike katika eneo lake.
Ndo maana tukasema mkichagua chama Cha Wakulima tunawaondoa wakuu wa Mikoa,Wilaya na Makatibu tarafa wote nchi nzima, kwasabubu tumetazama hatuajaona kwa viongozi hawa Wananchi mnaenda kupata huduma gani!..hivi ni vyeo vya kisiasa tu "amesema Rai
Tunataka Taifa ambalo kila mtu anufaike na Misha yake, hatuwezi kuvumilia mtu anaitwa kiongozi wa Serikali lakini hatuoni kazi yake anayoifanya ya kuhudumia watu kwa mujibu wa sheria.
Pesa zote za miradi ya maendeleo zinazotoka hadhina kuja kwenye Halmashauri za Wilaya mdhibiti wake ni Mkurugenzi wa Halmashauri husika na ndio msomi anae aminika lazima awe mchumi, sasa huyu Mkuu wa Mkoa mwenzangu na mimi wa darasa la saba anawezaje kumsaidia rais katika Matumizi ya pesa zinazoenda kwenye Halmashauri kwa ajili ya miradi?,
atamsimamia mtu mwenye digrii ya uchumi mwenye darasa la saba tu na siasa za CCM kuhotubia hotubia tu, utaweza kumgusa Mkurugenzi mwenye Elimu yake? matokeo yake miradi yote inayowekezwa huku chini inapingwa .A
amesema Rai.
RAI ACHUKIZWA NA UGATUZI WA MADARAKA.
Reviewed by mashala
on
13:31:00
Rating: 5

No comments
Post a Comment