CHUM AWAOMBA WANANCHI WA TANDAHIMBA KUJITOKEZA KWA WINGI KUPIGA KURA ZA NDIO KWA AAFP OKTOBA 29 MWAKA HUU.
Mgombea mwenza wa urais kupitia Chama Cha Wakulima (AAFP)Chum Abdallah Juma amewaomba Wananchi wa Tandahimba kujitokeza kwa wingi kukipigia kura za ndio chama hicho ili kiweze kushika dola nakuleta mabadiliko makubwa ya kiuchumi na kijamii.
Amesema hayo Septemba 23,2025 katika Viwanja vya forodhani Wilayani Tandahimba Mkoani Mtwara wakati akinadi Ilani ya AAFP kwa Wananchi nakuwaomba kukipigia kura za ndio,ili kuondoa kero zinazowakumba ikiwemo huduma za kijamii kama vile Maji,afya,umeme,pamoja na masoko.

"Nawaomba sana Wananchi mjitokeze tarehe 29 mwaka huu kukipigia kura za ndio chama cha AAFP,kwani sera zetu ni nzuri na zinalenga kuinua makundi yote ikiwemo wakina mama wenzangu pamoja na Vijana " amesema Mheshimiwa Chum.
Nakusisitiza kwamba"nichagueni mimi(Chum Abdallah Juma)mgombea mwenza,pamoja na Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kunje Ngombale Mwiru,ili tukasaidiane kuunda Serikali ambayo itakua na uchungu na rasilimali za nchi pamoja na kutatua kero zinazowakabili.
No comments
Post a Comment