AAFP KUWAONDOA NGUVU ZA KIUME WABAKAJI NA WALAWITI.
Mwenyekiti wa Chama Cha Wakulima (AAFP)Shani Kitumbua amesema kuwa endapo chama hicho kitashika dola kitahakikisha kinamuondoa nguvu za kiume mwanaume yeyote atakaekutwa na hatia ya kubaka au kulawiti ili kumfanya asitende tena kwa mwingine.
Kauli hiyo ameitoa Septemba 23,2025 wakati akizungumza na Wananchi wa forodhani Wilayani Tandahimba Mkoani Mtwara kwenye kampeni za kumnadi Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama hicho.
"Ndugu zangu tunajua sasahivi hali ya hewa imebadilika,wazazi wenzangu leo hii watoto wa kiume wanalindwa kuliko mtoto wa kike,watoto wa kiume ushoga umejaa sana,mlinde sana mtoto wako wa kiume usiwe bize na kulima,wala kitu kingine,watoto wanatekwa na wanaowateka wanaondoka nao sijui wanawapeleka wapi!"ameongea kwa kusikitika Kitumbua.
Kitumbua ambaye pia ni Mgombea ubunge jimbo la Chamazi Mkoani Dar es salaam,ameongeza kuwa"sisi kama Serikali ya AAFP tunataka kwamba mtu yeyote atakae kamatwa na kosa la kubaka au kulawiti tunamtoa nguvu za kiume kwasababu akishafungwa miaka thelathini tunawajaza wangapi,na wakienda huko magerezani wanaenda kubaka tena.
Akizungumzia changamoto zizaowakabili Wananchi wa Tandahimba,Bi.Kitumbua amesema kuwa wananchi hao wanakumbwa na matatizo mbalimbali ikiwemo katika masuala ya Kilimo,Afya,Maji,licha ya Serikali ya CCM kujinasibu kuwa imefanya maendeleo makubwa."Tunajua changamoto zipo nyingi sana,CCM na Serikali yake imetutesa sana,tumefika hapa forodhani maji hayapatikani huku Serikali ikisema imemtua mama ndoo kichwani kumbe ni uongo mtupu,maana ya kumtua mama ndoo kichwani ni kuwepo kwa huduma ya Maji katika kila nyumba na sio kuenda kuchota mbali ndio unaleta nyumbani"amesema
No comments
Post a Comment