Zinazobamba

AAFP KINA DHAMIRA YA DHATI KUWAINUA WAKULIMA KIUCHUMI:RAI

Na Mussa Augustine.Mtwara.


Katibu Mkuu wa Chama Cha Wakulima (AAFP )Rashid Rai amewaomba wananchi wa Wilaya ya  Tandahimba Mkoani Mtwara kukichagua chama hicho kwani kina dhamira ya dhati ya kuwainua wakulima kiuchumi.

Amesema hayo leo Septemba 23,2025 Walayani humo wakati akimnadi Mgombea wa urais wa chama hicho Kunje Ngombale Mwiru,na Mgombea mwenza Chum Abdalah Juma,kwenye mkutano wa kampeni uliyofanyika katika viwanja vya forodhani,nakubainisha kuwa wakulima wamekua wakidhalaulika na kukosa thamani toka Tanzania ipate uhuru mwaka 1961.
"Mkituchagua sisi(AAFP) mmejichagua wenyewe kwasababu toka uhuru wa nchi hii wakulima ndio kundi ambalo mnaishi katika mazingira magumu kuliko makundi mengine,mbaya zaidi kazi zote zinazofanywa na wakulima hazina thamani mbele ya wenzetu" amesema Rai

Nakufafanua kuwa "Leo una andaa shamba,unatafuta mbegu,unahudumia kwanzia mwanzo mpaka kwenye kuvuna lakini bei anakuja mtu anaitwa waziri ndio anapanga bei ya kuuza,yaani inafika mahala yeye yupo Dar es salaam au Dodoma anatangaza msimu wa kilimo 2025/26 Korosho daraja la kwanza(grade one)itauzwa bei fulani na daraja la pili (grade two)itauzwa bei fulani."
Aidha ametolea mfano nchini Uingereza nakusema kuwa nchi hiyo miaka kama 150 iliyopita ilitokea tatizo kati ya wafanyakazi wa sekta mbalimbali kuhusu maslahi yao ya mishahara iliyokua ikipangwa na Serikali,hivyo wafanyakazi hao waliamua kuanzisha chama chao cha siasa (Labour Party),

ambapo baada chama hicho kushinda kwenye uchaguzi mkuu wa nchi hiyo,wakati rais kupitia chama hicho akiapishwa alitangaza rasmi kiasi cha kima cha chini cha mshahara,wafanya kazi wote waliofanya kazi kwenye Viwanda vya nguo lazima wapatiwe lita moja ya maziwa kutoka kwa waajiri wao,kupata likizo ya kazi pamoja nakutenga siku maalumu ya wafanyakazi duniani( May mosi) na wafanyakazi wakawa na heshima.
Aidha amesema kuwa kutokana na hatua hiyo,AAFP kimeanzishwa kwa lengo la kuondoa shida mbalimbali za wakulima nchini Tanzania,ambao wanaonekana hawana thamani na huku ndio kundi muhimu ambalo linazalisha mazao ya chakula na biashara nakuipa heshima Tanzania na dunia kwa ujumla.

Aidha amewambia Wananchi kuwa endapo watamchagua  Kunje Ngombale Mwiru kuwa rais wao matatizo yote ya kudhulumiwa wakuliama yataisha kwasababu watakua  na Serikali yao wenyewe.

"Siku hizi kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,siku ukisikia inapigwa bajeti ya Kilimo ule muda Waziri anasoma bajeti ya kilimo watu wanaenda kuvuta sigara,watu wanaenda kunywa chai kwenye mgahawa,yaani manaake bajeti inayoitishwa haina maana kwao,ndio maana hakuna hata mwaka mmoja tumesikia  bajeti ya kilimo iko juu ,kila mwaka Wizara ya Kilimo ndio yenye bajeti ndogo kuliko Wizara zingine." amesema Rai.
Nakusisitiza kuwa," Sisi AAFP tunasema mtu yeyote anaeitwa waziri wa kilimo kazi yake itakua ni kutafuta masoko,wakati wa kilimo ukifika kazi yake nikutafuta masoko ulaya kabla ya Wakulima hawajazalisha ili msimu wa uandaaji wa mashamba ukifika ni wajibu wake kusema kwamba nimekwenda India wanataka Mbaazi,China wanataka Choroko,Japan wanaka Korosho,kwahiyo mwaka huu kwenye soko la dunia wanataka zao hili na hili,ili watu wetu wanapolima walime zao ambalo soko lake lina uhakika."

No comments