MWENYEKITI CCM KATA YA CHANIKA AREJESHA FOMU YA KUTIA NIA KUGOMBEA UBUNGE UKONGA.
Na Mwandishi Wetu.
Mwenyekiti wa CCM kata ya Chanika William Abas Mwila amerejesha fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Ukonga.
Mwila amekabidhi barua fomu hiyo leo Julai 2 ,2025 kwa katibu wa CCM Wilaya ya Ilala Chief Sylvester Yaredi baada ya kukamilisha taratibu
Aidha amebainisha kwamba amejitathimini na kuona kuwa anajitoshereza kutatua changamoto zinazowakabila wananchi wa Ukonga .
Amesema kwamba yupo tayari kuwatumikia Wananchi,nakwamba Wanaukonga watakua wamepata Kiongozi atakaesikiliza kero za muda wowote.
No comments
Post a Comment