MFANYABIASHARA DAUD IKWABE ALITAKA JIMBO LA KIVULE.
Kada wa CCM Daud Ikwabe amechukua na kurudisha fomu ya kutia nia kugombea Ubunge Jimbo la Kivule.
Ikwabe amerudisha fomu hiyo leo Julai 1,2025 kwa katibu CCM Wilaya ya Ilala Chief Sylvester Yaredi.
Amesema ameamua kugombea nafasi hiyo ili kumsaidia Rais Dkt. Samai Suluhu Hassan kuwaletea maendeleo wananchi wa Kivule.
Aidha amesema kuwa endapo atapata ridhaa ya kuwa Mbunge wa Jimbo hilo atahakikisha anatatua changamoto za muda mrefu ikiwemo miundombinu ya Barabara.
No comments
Post a Comment