MHARIRI RADIO UHURU AREJESHA FOMU YA KUTIA NIA KUGOMBEA UBUNGE KIVULE
Mjumbe Halmashauri Kuu CCM Taifa Mstaafu na Mhariri wa habari Radio Uhuru,Angelina Akilimali amechukua na kurejesha fomu ya kugombea Ubunge Jimbo la Kivule.
Angelina amerejesha fomu hiyo leo Julai 1,2025 kwa Katibu wa CCM Wilaya ya Ilala Chief Sylvester Yaredi.
Ameshukuru viongozi wa chama chake cha CCM kwa kuweka Mazingira rafiki ya kidemokrasia,kwa kunilea kisiasa hadi kufikia hatua hiyo.
Amesema kwamba amechukua fomu ya kuwania kugombea nafasi ya Ubunge Kivule si kwa kutafuta madaraka bali kwa nia njema ya kuwatumikia wananchi wa Jimbo la Kivule kwa moyo wa dhati,kwa bidii nakwa maono mapya ya maendeleo ya Jimbo la Kivule.
No comments
Post a Comment