Zinazobamba

KAMISHNA WA UHIFADHI NCAA AWASHUKURU WADAU WA SEKTA YA UTALII


Na Mwandishi Wetu.

Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro (NCAA) Bw. Abdul-Razaq Badru kupitia mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika jijini Arusha tarehe 30 Juni, 2025 amewashukuru Watanzania, Wadau wa Sekta ya Utalii na wageni mbalimbali waliotembelea eneo la hifadhi ya Ngorongoro kwa kuipigia Kura hifadhi hiyo na kuiwezesha kutangazwa kuwa Kivutio bora cha Utalii Barani Afrika mwaka 2025.Hafla ya kutangaza washindi wa tuzo hizo zinazoratibiwa na  Mtandao wa World Travel Awards (WTA) ilifanyika tarehe 28 Juni, 2025 Jijini Dar es Salaam.



No comments