Zinazobamba

UPDP YAIOMBA TAMISEMI KUONGEZA MUDA WA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA

Na Mussa Augustine.

Chama Cha United People Democrat Party, (UPDP) kimeiomba Serikali kupitia TAMISEMI kuongeza muda wa uchaguzi wa serikali za mitaa kutokana na muda uliopangwa wa siku sabu kua hautoshi.

Akizungumza na Wanahabari  jijini Dar es Salaam  Mwenyekiti wa chama hicho Taifa,Ibrahim Kadege amesema kwamba muda wa siku saba hautoshi kwasababu vyama hivyo havina ruzuku hivyo vinashindwa  kumudu gharama za maandalizi ya uchaguzi huo ikiwemo masuala ya kampeni

"Tunaiomba Wizara yenye mamlaka iongeze muda ,muda wa siku saba hautoshi kutokana na vyama vyetu kukosa fedha za kuweza kufanya Kampeni maeneo mbalimbali kwa wakati" amesema Kadege

 Akizungumzia kuhusu maandamano ya CHADEMA yaliyopangwa kufanyika siku ya Jumatatu Septemba 23, 2024, Kadege amesema kwamba maandamano hayo hayataleta suluhu ya vitendo vya mauaji ,nakuwasihi viongozi wa chama hicho, kufanya mazungumzo ya amani na Serikali ili kufikia muafaka. 

"Rais Dkt. Samia ameagiza vyombo vya usalama vifanye uchunguzi haraka nakumpatia taarifa za vitendo mbalimbali vya utekeji na mauaji ,hivyo tusubiri taarifa itabainisha kwa kina nani waliyehusika,endapo wasipochukuliwa hatua ndipo tutaona nini cha kufanyika" amesisitiza.Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu  wa chama hicho, Ally Hoza amesema kuwa vitendo vya mauaji vinazidi kushamiri kutokana na Wajumbe wa Nyumba 10, kutokushirikishwa katika kuwatambua watu wanaohamia kwenye maeneo yao.

"Viongozi wa Serikali ya Mitaa washirikishwe katika kuwatambua wapangaji wanaopanga kwenye nyumba zetu,tujue kama ni raia wa Tanzania na maeneo yao wanayotoka,hii itasaidia kudhibiti vitendo vya mauaji na ukatili kwa jamii " amesema Hoza


Hakuna maoni