Zinazobamba

TASISI YA SAMABAZA UPENDO YATOA MISAADA MBEZI LUISI

Na Mussa Augustine 

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo amechangia Shilingi milioni moja  katika taasisi ya Sambaza Upendo ambayo iko chini ya Dkt. Askofu Leonard Ntibanyiha wakati wa hafla  ya kugawa misaadakwa watu wenye uhitaji iliyofanyika katika Kanisa la Goran, Mbezi Luisi jijini Dar es Salaam.

Fedha hizo zimetolewa  Septemba 21, 2024 na  Ofisa Mazingira wa Manispaa hiyo, Nice Vahaye kwaniaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo,katika kuchangia shughuli ya kutoa misaada kwa wakazi wa Mtaa wa Matope, Mbezi Luis, wanaoishi katika mazingira magumu wakiwemo wajane, wazee na  yatima akimwakilisha Mkurugenzi  wa Manispaa ya Kinondoni.

“Nimekuja mwakilisha Mkurugenzi wetu, kwa hakika tumeona juhudi zinazofanywa na Taasisi ya Sambaza Upendo na kutokana na changamoto ambazo wamezisema hapa ikiwemo ukosesefu wa eneo la kujenga Kituo na Shule, ukosefu wa gari na nyingine, yote kwa pamoja ni fedha, hivyo natoa sh. ml 1.

“Pia tutaendelea kushirikiana katika kuhakikisha juhudi hizo zinaendelea kuhimalika kwa maslahi ya watanzania wote hususan kwa wanaoishi katika mazingira magumu na kwa kufanya hivi tutawaondelea mawazo maovu na amani itadumu milele na hiyo ndio nguzo yetu,” amesema

 Pia Mchungaji Aman Kayuni, wa Taasisi ya Sambaza Upendo ametanabaisha kwamba lengo la kusambaza upendo ni kuingiza matendo kwa kubeba agizo la Mungu, linalosema “Nendeni mkayafanye mataifa yote yakawe wananafunzi”.

“Pia Yesu anasema,  mkihudumia hawa mmenihudumia mimi”  na kwa namna hiyo kwa jina la Yesu ambalo ndio msingi na upendo wa msalaba uliosababisha akafa msalabani kwa namna moja au nyingne inatulazimu sisi Sambaza Upendo, kuwakusanya watu kila tunapojaaliwa kuweza kuwahudumia, kwa neno, kwa chakula na mahitaji mengine kwa namna tunavyoweza kushauriana”, amesema.

 Akizungumzia masuala yanayojiri Kwa Sasa ya utekaji, mauaji, amesema Yeu alitumia neno kuponya mioyo ya watu, hivyo moyo ya watu usipopata neno ni ngumu kutengenezeka kibinadamu, kinachotakiwa kwa jamii ni kuvua utu wao wa zamani na kuvaa mpya hivyo ndivyo Mungu atakavyoondoa hali ya mauji, uvivu .

“Ombi letu kwa jamii, wanatakiwa wajikite zaidi katika neno la Mungu ili kuondoa roho ya utekaji, mauji, ubakaji, neno la Mungu likiingia katika mioyo ya watu biblia inasema,  neno ni moto inayoyayusha roho ovu na hazitaweza kuwepo”, amesema.

Naye Mwenyekiti wa Wajane, Wilaya ya Ubungo, Josephine Eliazari, amesema wanayofuraha kujumuishwa pamoja na kupatiwa misaada mbalimbali na kutoa wito kwa wadau wengine kujitokeza kufanya hivyo na si kuwaachia jukumu hilo, taasisi ya Sambaza Upendo.

Taasisi ya Sambaza upendo, Septemba  21,2024 iliendelea na utaratibu  wake wa kugawa misaada ya mahitajia katika maeneo mbalimbali  Nchini humo,ikiwemo watu wasiojiweza kama vile watoto yatima, wajane, na wazee 


Hakuna maoni