Zinazobamba

DOYO AFUTA KESI MAHAKAMA KUU


Na Mussa Augustine.

Aliyekua Mgombea nafasi ya uenyekiti Taifa Chama Cha Alliance For Democratic Party(ADC )Doyo Hassan Doyo ameifuta  kesi ambayo alifungua Agost 16 Mwaka huu, katika Mahakama kuu kwa ajili ya kupinga taratibu zilizotumika katika  uchaguzi huo ambao ulimpa ushindi mgombea mwenza Shaaban Matutu.


Doyo ambaye kwa sasa ni Katibu Mkuu wa Chama Cha National League for Democracy (NLD) amefikia uamzi huo leo Septemba 25,kutokana na kushauriana na wanasheria wake pamoja na  Viongozi wenzake waliokubaliana kufungua kesi hiyo.

Akizungumza  katika mahojiano maalumu na Kituo hiki leo Septemba 25,2024  Jijini Dar es salaam  Doyo amesema kwamba kesi hiyo ilikua ni kupinga taratibu za uendeshaji wa uchaguzi huo,pia kwenye kesi hiyo alishtaki kamati ya rufaa kushindwa kujibu rufaa yake kwa wakati.

Aidha amesema kuwa walifungua kesi hiyo ili Mahakama iweze kutafsiri yale malalamiko ya uvunjifu wa katiba ya chama,kanuni ya uendeshaji ya chama na kanuni ya uchaguzi ya chama kwa namna taratibu ambavyo zimevunjwa wakati wa uchaguzi wa viongozi wa chama ndani ya chama Cha ADC.

"Leo ilikua kesi kati yangu na Hamad Rashid Mohamed na Viongozi wa chama Cha ADC, ambao walipita kwa mizengwe katika Uchaguzi wa chama uliopita ,nikafungua kesi mahakama kuu tarehe 16,08,2024  ,kesi ilikua isikilizwe leo tarehe 25,bahati nzuri nikashauriana na wanasheria wangu,Viongozi na wanachama wenzangu ambao tulikubaliana kufungua kesi hiyo Wameshauri kesi hiyo kuachana nayo kwasababu tupo katika Maisha mengine tumehamia chama Cha NLD." amesema

Ameongeza kuwa "kwasasa tunaendelea na mipango mingine ya kuhakikisha chama cha  NLD kinaimarika,hivyo tumeona tuwape nafasi ADC nao waendelee na siasa kuliko kuendelea nao mahakamani ,kwahiyo tumewaacha wafanye ambayo yatakisaidia chama chao wasije wakashindwa baadae  wasingizie kesi,tupo katika kipindi cha kuelekea  uchaguzi.

.Kuhusu Gharama za kesi.

Akizungumzia kuhusu Gharama za kesi Doyo amesema kwamba hadai gharama yoyote kwa ajili ya uendeshi wa kesi hiyo,ambapo kesi hiyo ilikua igharimu jumla ya kiasi cha  shilingi milioni 30 ,nakwamba malipo ya awali amelipa kiasi cha shilingi milioni 7 .

" Hizo ni gharama za kukuza Demokrasia,mimi kwa upande wangu siwezi kudai chochote hizo ni sehemu ya matumizi yangu ya kawaida ,nimeshazipoteza zile pesa kama ninavyopoteza pesa wakati wa ujenzi wa chama kwasababu vyama tulivyonavyo havina ruzuku tunaviendesha kwa gharama ya pesa tulizo nazo." amesema.

.Uchaguzi Serikali za Mitaa.

Katibu Mkuu huyo wa NLD amesema  kwamba Viongozi wa juu wa chama hicho tayari wameshatoa maelekezo kwa viongozi Nchi nzima ya kusimamisha wagombea wa Serikali za Mitaa ,Vijiji na Vitingoji kwa ajili ya maslahi ya chama nakwamba Chama hicho kimejipanga kuhakikisha kinasimamisha wagombea kadri itakavyowezekana katika maeneo ya Nchi.

" Tunawahamasisha kujiandikisha lakini tutaweka mawakala wetu ili kuhakikisha namba inayoandikisha katika Mitaa ni namba sahihi ili tuweze kua na wapiga kura sahihi katika uchaguzi huo,hivyo natoa rai kwa wanachama wote na Viongozi wa NLD Nchi nzima wahakikishe  wanaweka wagombea wa Serikali za Mitaa,Vijiji na Vitingoji  sehemu zote ambazo chama hicho kipo.

.Ruzuku kwa Vyama Vya Siasa.

Doyo amesema kwamba ifike hatua Vyama vya Siasa visivyo na ruzuku viache utaratibu wa kulilia ruzuku,vijipange kufanya kazi za kisiasa ili viweze kujikomboa kwa kupata wabunge au kura nyingi za ubunge,kwani ruzuku ile imetungwa kwa mujibu wa sheria ina vigezo vyake vya kupatiwa ambapo lazima chama kifikishe kura asilimia 5 za wabunge,ama kura asilimia 5 za rais,au kupata wabunge ama madiwani wengi.

" Mimi siamini kwamba ukiwa huna ruzuku huwezi kufanya siasa kwasababu hiki ni kizungumkuti haiwezekani serikali ikupe fedha  halafu ushindane nayo uishinde, hivi vyama vinavyopokea ruzuku vijitafakari" amesisitiza Doyo.



Hakuna maoni