Madrasa zetu haziko salama, Sheikh Masoud
Mnamo tarehe 02/02/2024 Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania iliamua kuifunga Madrasa ya Al Habash iliyokuwa maeneo ya Sogea Mbele
na Nkuhungu, Dodoma katikati mwa Tanzania kwa tuhuma za kutoa huduma ya elimu
katika mazingira hatarishi. Madrasa hiyo ilikuwa na jumla ya wanafunzi wa kike
takribani 132 wenye umri wa kati ya miaka 13 hadi 20 katika maeneo yote mawili,
wanafunzi hao walikuwa wanatoka maeneo tofauti hususan ndani ya mkoa wa Dodoma.
MAONI:
Tunalaani vikali uamuzi huu usiokubalika wa serikali wa kuifunga
madrasa ya Al-Habash bila sababu za msingi. Inaonekana kuwa serikali ilichukua
hatua kama sehemu ya muendelezo wa kampeni ya kimataifa dhidi ya Uislamu.
Sababu zilizotajwa hazina mashiko kwa serikali kufikia uamuzi huo. Wakati hayo
yakijiri, siku chache baadae, tarehe 06/02/2024 serikali iliuvunja msikiti wa
wanafunzi katika shule ya sekondari ya Tawalanda iliyopo Bagamoyo mkoani Pwani.
Kampeni ya Kibepari kimataifa ya chuki dhidi ya Uislamu ambayo
inasukumwa hasa na Marekani inatumia visingizio mbalimbali kudhibiti, kuingilia
kati na kufunga vyanzo vya elimu ya Kiislamu. Hili linafanyika katika ulimwengu
wote wa Kiislamu katika zikilengwa Madrasa zenye mfumo wa kiasilia, vyuo vya
kati au vyuo vikuu vya Kiislamu.
Ndani ya mwaka 2015 takriban wanafunzi 147 katika Wilaya ya Hai,
Kaskazini mwa Tanzania waliokuwa wakisoma katika Madrasa ya misikiti mitatu:
Masjid Bilal (Kibaoni), Masjid Othman (Uzunguni) na Masjid kwa Kiriwe waliwekwa
kizuizini na vyombo vya dola. (Mtanzania 2 Aprili 2015). Pia katika mwaka huo
huo mwalimu wa madrasa, Al-haji Maulana Shiraz (71) wa jumuiya ya
Zawiyatul-Qaadiriya katika Wilaya ya Masasi Kusini mwa Tanzania alikamatwa
akiwa na wanafunzi 11 tu kwa kisingizio cha vita dhidi ya ugaidi. (Habarileo, 3
Aprili 2015).
Mabepari wakoloni wa kimagharibi walitengeneza propaganda (ya
vita vya ugaidi) zinazosababisha mgawanyiko, kuyumbisha kwa watu kijamii na
kiuchumi, kueneza chuki, na mara nyingi waendesha mashtaka hushindwa kuleta
ushahidi mbele ya mahakama dhidi ya madai ya ugaidi, hata baada ya miaka mingi
ya kile kinachoitwa "upelelezi".
Zaidi Endelea hapa:HATA MADRASA ZETU HAZIKO SALAMA CHINI YA UBEPARI
Hakuna maoni
Chapisha Maoni