WAISLAM WAONYWA,WAAMBIWA MANENO KUNTU,SOMA HAPA KUJUA
Katibu Mkuu wa Dini ya Kiislam nchini Sehk Khamis Matanga akisoma Tamko mbele ya Waislam |
NA EXAUD MTEI
Waumuni wa dini ya kiislam na dini nyingine nchini Tanzania wametakiwa kuahikikisha kuwa hawaruhusu aina yoyote ya chuki za kidini ambazo zitapelekea kutokuelewana na kuleta machafuko hususani kipindi hiki ambacho Tanzania iko katika mambo muhimu ya uchaguzi mkuu.
Wito huo umetolewa leo Jijini Dar es salaam katika kongamano la kidini la siku mbili lililoandaliwa na taasisi ya kiislam ya IMAM BUKHARY ISLAMIC FOUNDATION kongamano ambalo linawahusisha viongozi mbalimbali wa dini tofauti nchini Tanzania.
Waislam wakimsikiliza kwa Makini kwa makini |
Akifungua kongamano hilo leo mgeni rasmi ambaye ni katibu mkuu wa tasisi za kiislam Tanzania shekh KHAMIS MATAKA amesema kuwa tofauti za kidini baina ya watanzania sio chanzo cha kusababisha vurugu na uvunjifu wa amani bali ni moja ya njia ya kuwaunganisha watanzania na kuwafanya wawe kitu kimoja.
Amesema kuwa machafuko mengi ambayo huwa yanatokea katika nchi mbalimbali duniani husababishwa na chuki za kidini ambazo hupandikizwa na mataifa makubwa kwa lengo na kuwagombanisha ili wao waweze kuingia kwa urais jambo ambalo amesema kuwa ni la kupiga marufuku mara moja .
Askofu FILBERT MBEPELA ambaye ni mmoja kati ya viongozi wa dini za kikiristo waliohudhuria kongamanno hilo akizungumza. |
Aidha amesema kuwa kuelekea kipindi hiki cha uchaguzi sio kipindi cha viongozi wa dini kujiingiza katika siasa kwa kuwapigia debe baadhi ya wagombea bali ni kipindi cha viongozi wa dini kukaa pamoja na kutumia dini zao kuliombea taifa na kuacha mambo ya siasa kuendeshwa na wanasiasa wenyewe tofauti na sasa ambapo kumeonekana wazi kuwa kuna muingiliano wa viongozi wa dini kuingia katika maswala ya siasa.
Aidha akizungumza kwa niaba ya viongozi wa kikristo waliohudhuria kongamano hilo askofu FILBERT MBEPELA amesema kuwa huu ni muda wa dini zote nchini kuungana kwa pamoja kulitetea taifa la Tanzania na kuepuka chuki na fitna ambazo mwisho wake zitaleta madhara makubwa kwa taifa yakiwemo mauaji yasiyo ya haki.
Hizi ni baadhi ya piocha ambazo zinaonyesha madhara ya chuki za kidini ambazo mwishowe huzalisha vutrigu na mauaji makubwa katika mataifa mbalimbali |
Kongamano hilo litafanyika siku mbili ambapo lengo kuu ni kuwakutanisha viongozi wa kiislam na baadhi ya viongozi wa dini nyingine mbali mbali kujadili hali ya amani duniani na kuona jinsi kgani Tanzania inaweza kuepuka machafuko ya kidni kama yawayowakuta mataifa mengine kama Iraq,Libya,Syria na nchi nyingine za kimagharibi.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni