Zinazobamba

FCS NA LATRA CCC ZATIA SAINI MAKUBALIANO YA KUMLINDA MTUMIAJI WA HUDUMA ZA USAFIRI ARDHINI.

Mkurugenzi Mtendaji wa FCS Justice Rutenge(kulia) kushoto kwake ni Katibu Mkuu Latra ccc Daud Daud wakitia Saini makubaliano ya Miaka mitatu ya kuwezesha Mradi wa kulinda watumiaji wa huduma sa usafiri ardhini

Na Mussa Augustine.

Foundation For Civil Society (FCS) imengia makubalino na baraza la ushauri la watumiaji huduma za  usafiri ardhini (LATRA CC) kwa ajili ya kutekeleza mradi wa miaka mitatu wa  kulinda huduma za watumiaji wa usafiri wa ardhini.

Akizungumza leo Oktoba 22,2024 Jijini Dar es salaam ,mara baada ya kutia saini ya makubaliano hayo Mkurugenzi Mtendaji wa FCS Justice Rutenge  amesema kuwa ubia huo unaendana na  misingi  ya FCS,nakwamba miezi kadhaa iliyopita FCS ilitiliana saini ya  makubalino na Baraza la Ushauri la watumiaji wa huduma za  mawasiliano (TCRA CCC).

"Leo tunaongeza mkataba baraza lingine moja ( LATRA CC) ikiwa ni sehemu ya kuwezesha baraza hili liweze kuwa na uwezo kiutendaji kwa ajili ya kuwahudumia wananchi wanaotumia usafiri wa ardhini" amesema Rutenge

Nakuongeza kuwa,"Ubia huu unaenda na misingi inayotuongoza kuwezesha ushirikiano kwa ajili ya maendeleo,ndani ya hiyo nadharia tunaamini hakuna maendeleo ambayo yanaweza yakafanywa bila watu kushiriki kuna vyombo vimewekwa kisheria ambavyo vinapaswa kusaidia ushiriki wa wananchi katika michakato mbalimbali ya  maendeleo.

Rutenge amesema baraza hilo ni muhimu katika suala hilo hasa hasa katika usafiri wa ardhini,ambapo ni jambo muhimu katika maendeleo ya nchi,pia ni  uti wa mgongo wa biashara kwa sababu bila usafiri thabiti wa ardhini bidhaa haziwezi kutoka viwandani kwenda sokoni.

Halikadharika amesema kuwa  usafiri ni kiungo muhimu katika utoaji wa huduma  za maendeleo, akitolea mfano huduma za usafiri katika vituo vya  Afya, shuleni,sehemu ya kupata maji safi na salama.

"Kwa ujumla tunaweza kusema bila miundombinu ya usafiri imara inakua vigumu sana kwa Taifa kufikia malengo ya maendeleo endelevu, malengo haya hatuwezi kuyafikia kama hatuna mifumo ya usafiri ambayo inaeleweka, hivyo huu ushirikiano wetu na Latra ccc ni sehemu muhimu sana ya kuhakikisha miundombinu inaimarishwa na inatumiwa vyema kwa manufaa ya kila mtanzania  hasa wanaotumia biashara na usafirishaji katika maisha yao.
Naye katibu mkuu baraza la ushauri la watumiaji wa huduma za usafiri wa ardhini  (LATRA CCC) Daud Daud amesema kuwa Ushirikiano huo umelenga kufanya miradi ya pamoja katika kuongeza uwezo wa kiutendaji ili kutoa huduma bora kwa watumiaji wa usafiri wa ardhini.

"Mradi huu tunautekeleza hasa katika maeneo makubwa mawili,eneo la kwanza ni kutengeneza miradi kwa pamoja na kutekeleza kwa pamoja, eneo la pili ni kutoa Elimu kwa watumiaji wa huduma za usafiri wa ardhini, pamoja na kujiongezea uwezo sisi watendaji ili kutoa huduma inayoendana na wakati" amesema Daud 




Hakuna maoni