Zinazobamba

TANZANIA NA KAMPUNI YA CECIS LTD YA CHINA ZAKUBALIANA KUWEKEZA KATIKA MIFUMO YA TEHAMA

                   Maryprisca Mahundi

Na Mussa Augustine.

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, leo Oktoba 21, 2024, imesaini makubaliano ya uwekezaji na mafunzo na Kampuni ya Huduma za Mawasiliano ya Kielektroniki ya China (CECIS LTD),ili kuongeza ujuzi kwa vijana wa Kitanzania na kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha utengenezaji wa kompyuta duniani.

Akizungumza mara baada ya utiaji saini huo Naibu Waziri wa Wizara hiyo Maryprisca Mahudi amesema kuwa uwekezaji huo utaisadia Tanzania kuimarika kiteknolojia kwenye mifumo ya Tehama nakwamba Vijana wengi watapata ajira.

Amesema kuwa kupitia makubaliano hayo, zaidi ya makampuni 600 ya utengenezaji wa vifaa vya kompyuta yataweza kuwekeza nchini Tanzania,hivyo fursa za kiuchumi wa kidigitali zitaongezeka.

Makubaliano hayo yamesainiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mohammed Abdulla, pamoja na Mwenyekiti wa Kampuni ya CECIS, Guo Zhaoping, huku yakishuhudiwa na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Maryprisca Mahundi.

“Makubaliano haya ni matokeo ya ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan nchini China aliyoifanya hivi karibuni,Kampuni hii ni wataalamu wa usalama wa mitandao, na hivyo wataalamu wa kitanzania watajifunza kutoka kwao, tukizingatia hitaji la wataalamu zaidi wa TEHAMA nchini,”emesema

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mohammed Abdulla, amesema kuwa uwekezaji huo utatoa fursa kubwa kwa Watanzania kujifunza, kupata ajira, na kujiendeleza katika sekta ya teknolojia ya Tehama.

Nae Mwenyekiti wa CECIS, Guo Zhaoping, ambaye pia ni Naibu Mkurugenzi wa Sayansi na Teknolojia wa kamati ya kampuni hiyo, amebainisha kuwa uwekezaji huo unafuata misingi ya ushirikiano wa Tanzania na China na unalenga kuchochea maendeleo ya uchumi wa kidijitali.

“Kampuni yetu inafanya uwekezaji katika maeneo makuu matano, ikiwemo sekta ya kompyuta na usalama wa mitandao,tunapofanya shughuli hizi za kibiashara, pia tunalenga kukuza uchumi wa kidijitali nchini Tanzania na katika nchi nyingine,” amesema  Zhaoping.Hali kadhalika Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya TEHAMA, Dkt. Nkundwe Moses Mwasaga, amesema kuwa sehemu ya makubaliano hayo ni kuvutia makampuni mbalimbali ya kielektroniki kuwekeza nchini. 

"Mmwaka 2025 kutakuwa na maonesho makubwa ya utengenezaji wa vifaa vya kompyuta Afrika, ambapo Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kupitia Tume yake watakuwa wenyeji wa maonesho hayo" amesema Dkt Mwasaga


Hakuna maoni