Zinazobamba

SERIKALI ITAENDELEA KUWEKEZA KWA USAWA KATIKA RASILIMALI WATU--RIZIKI PEMBE

                                   Mh.Riziki Pembe                 

Na Mussa Augustine

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mh. Riziki Pembe Juma ameseam Serikali itaendelea kuwekeza kwa Rasilimali watu kama nyenzo muhimu katika kufikia malengo ya Kitaifa na kukuza uchumi pamoja na kutoa huduma bora kwa wananchi.

Amesema hayo  leo Oktoba 21, 2024 Jijini Dar es Salaam wakati akifungua kongamano la nne la Wanawake katika Uongozi, nakubainisha kuwa Serikali imekuwa ikifanya jitihada ili kuhakikisha usawa wa kijinsia unazingatiwa katika mchakato wa uandaaji na utekelezaji wa mipango ya rasilimaliwatu, ajira pamoja na mafunzo.

Bi.Riziki amesema kuwa Serikali imekuwa ikizingatia usawa katika upandishwaji na ubadilishwaji vyeo kwa kada mbalimbali pamoja na urithishanaji wa madaraka, uteuzi katika nafasi mbalimbali za uongozi ili kupunguza tofauti za uwakilishi kati ya wanawake na wanaume katika maamuzi.

“Ushiriki wa wanawake katika ngazi za maamuzi na uongozi ni moja ya vipaumbele vya Serikali katika kuhakikisha usawa kati ya wanaume na wanawake, na takwimu zinaonyesha wanawake katika nafasi za uongozi wakiwemo Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu, Naibu Makatibu Wakuu na wakurugenzi katika taasisi mbalimbali za umma ni asilimia 28.6 ya viongozi wote” amesema

Ameeleza kuwa takwimu hizo zinaonesha ni kiashiria chanya kuelekea kufikia asilimia 30 ya uwakilishi wa wanawake katika uongozi, ambayo ni hatua muhimu kuelekea kufikia lengo Na. 5 la Usawa wa Kijinsia (SDG 5) kufikia asilimia 50 ifikapo 2030.

Amesema kuwa Serikali inatekeleza sera, mikakati na mipango mbalimbali ya maendeleo ikiwemo sera ya maendeleo ya wanawake na jinsia ya mwaka 2000 pamoja na mkakati wake wa 2005, mpango wa tatu wa maendeleo wa Taifa (2021/22-2025/26), na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025.

 “Pia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inatekeleza Dira ya Maendeleo ya Zanzibar ya Mwaka 2050, Mpango wa Tatu wa Maendeleo na Kupunguza Umasikini Zanzibar (MKUZA III), Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Mwaka 2030 pamoja na sera na mikakati mbalimbali ili kuimarisha usawa wa kijinsia na kuleta maendeleo jumuishi kwa wananchi” amesema Bi. Juma.

Ametoa pongezi kwa Taasisi ya Uongozi Institute kwa kuandaa kongamano ambalo linatoa fursa ya kubadilishana uzoefu na kujadili namna ya kuimarisha uongozi wa mabadiliko miongoni mwa viongozi wanawake. 

“Naishukuru Taasisi ya UONGOZI kwa kunialika katika kongamano hili muhimu, niwapongeze kwa kuandaa na kutekeleza programu hii muhimu ya mafunzo kwa viongozi wanawake, pia nawapongeza viongozi wote wanawake kwa kuchaguliwa kujiunga na awamu ya tano na sita ya programu hii” amesema                             Kadari Singo

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Uongozi Institute Kadari Singo amesema kuwa Kongamano hilo la kikanda linahusisha nchi mbalimbali za Afrika lengo ni kua na mjadala wa pamoja unaohusu mambo makubwa yanahusu wanawake na uongozi kuhusu wanawake viongozi na mbadiliko.

Amesema kuwa Kongamano hilo hufanyika Kila Mwaka ambapo ni Kongamano la nne ambalo huhusisha wanawake viongozi kutoka sekta mbalimbali katika nchi mbalimbali na hapa nina nchi kadhaa ambazo ni Malawi,Zambia,Ethiopia,Kenya,Uganda,Ghana, Cameroon,Msumbiji ,Afrika kusini na Botswana" amesema Singo

Nakuongeza kuwa " tunatamani kuendelea kuhusisha viongozi wengi lakini kwasababu ya ufinyu wa nafasi na baadhi wanahudhuria wakiwa katika katika mifumo yetu ya Mtandaoni( online).

Aidha ameendelea kufafanua kuwa tafiti zilizofanywa na Uongozi Institute zinaonesha kwamba wanawake wengi wapo katika nafasi za chini za utendaji ambapo kwenye nafasi za juu za maamuzi wanapungua.

"Tukasema kwamba labda tuongeze jitihada za kuwaweka kwenye program ili waendelee kua kwenye sifa za juu na umahili kwenye nafasi za maamuzi,hivyo katika Kongamano hili tumeleta wabobezi kwenye maeneo ya mijadala hiyo ambao watachangia kwenye mambo ya mabadiliko." Amesema

Aidha Singo amesema kwamba mafunzo hayo ni lazima yawe jumuishi ,maana yake nikwamba lazima na wanaume wahusishwe kwasababu tatizo halipo  kwa wanawake pekee bali wanaume pia ni sehemu ya tatizo.

"Mafunzo haya yameanza rasmi mwaka 2022 ,yamekua na wahitimu wapatao 199 ,ambapo Kwa Sasa ni darasa la 5 na 6 ambalo lina wanawake 100, ambao wanaanza mafunzo ya darasani kwa siku sita,baada ya hapo wanaingia kwenye program ya malezi na wakimaliza watasoma Vitabu ,nakufanya assignments nyingi baada ya miezi sita wale watakaofanikiwa watahitimu mwezi wa 5,2025." amesema

Nakuongeza kuwa,"Baada ya hapo tutakua na darasa jingine mwezi wa 10, 2025, awali program hii tulipotangaza wanawake takribani 1500 waliomba na kati yao wanawake 500 walionekana wana sifa lakini uwezo tulionao ni wanawake 100 ,hivyo tunaendelea kutafuta wafadhili kutoka vyanzo vingine ili tuendeleze wanawake wengi zaidi.

Aidha ameongeza kuwa kwasasa taasisi hiyo inapata ufadhili kutoka Jumuiya ya umoja wa ulaya( Europian Union) Serikali ya Finland,na Serikali ya Tanzania pamoja na UN Women,nakwamba kiasi cha Euro laki mbili na nusu zinalipwa kila Mwaka kwa ajili ya wanawake wanaopata mafunzo hayo.




Hakuna maoni