Mufti Zubeir alimwa barua ya wazi na waislam, kisa ni Bakwata kukaa kimya katika mambo mazito ya waislam
BARUA YA WAZI KWA MUFTI WA TANZANIA NA BAKWATA
BISMILLAHI RRAHMANI RRAHIYM
ASALAAM ALAYKUM,
YAH: UKIMYA AMMA KUANGAZIA VISIVYO QADHIA ZA WAISLAMU
Tunaandika waraka huu wa nasaha kwako Mheshimiwa Mufti na Baraza
Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) kwa kuwa dini ya Uislamu imehimiza kupeana
nasaha, kuamrishana mema na kukatazana mabaya. Na asili nasaha hizi na mfano
wake hupaswa kupewa Waislamu binafsi, taasisi, jumuiya nk. Bali sisi
tunazielekeza kwenu kwa nafasi yenu mbele ya Umma ndani ya Tanzania na Uislamu
kwa jumla.
Kwa hakika Ummah wa Waislamu nchini Tanzania unasikitishwa na
kuhuzunishwa kutokana na ukimya wenu wa kupita mipaka au kuangazia visivyo
katika qadhia kadhaa zinazowasibu Waislamu kitaifa na kimataifa.
Baadhi ya qadhia hizo ni kama hizi zifuatazo:
1. Mauaji ya kijidola bandia cha Israil kwa Waislamu wa Gazza na
Palestina kwa jumla:
Dhulma, mateso, ukatili na mauaji ya Israili kwa Waislamu wa
Palestina asili yamekuwepo kwa miaka 75, lakini yameshitadi zaidi katika hali
isiyoelezeka baada ya tukio la mujahidina wa Hamas wanaopigana kujihami (Jihadi
diffai) kuingia ndani ya Israil. Mheshimiwa Mufti na BAKWATA kwa kuweka kwenu
kumbukumbu sawa, qadhia ya Palestina ina mafungamano ya moja kwa moja kwanza na
aqiida ya Kiislamu. Masjid Aqswa ndio qibla cha mwanzo cha Waislamu, kituo cha
Safari ya Miujiza ya Mtume SAAW (Israi na Miiraj) na taadhima ya eneo hilo
kwani ni sehemu ya eneo la Biladu Shaam. Bali fiqhi ya Kiislamu inalihesabu
eneo hilo ni eneo la Umma baada ya kufanyiwa fat-hi na Khalifah Umar Al-Khattab
mwaka 17 Hijria/ 638 Miladi. Mauaji haya ya karibu ya Israili yanayoambatana na
Waislamu wa Palestina kuzuiliwa kila kitu kuanzia maji, chakula, matibabu nk.
yamekuwa yakiendelea mfululizo kwa karibu miezi minne sasa huku sehemu kubwa ya
dunia kuanzia baadhi ya nchi, wanaharakati, wanaopenda haki, utu na uadilifu
Waislamu na wasiokuwa Waislamu wamekuwa wakipaza sauti zao kupinga, kulaani,
kufedhehi dhulma, uharamia na ukatili unaotendwa na kijidola cha Israili. Kwa
hapa Tanzania tumeona hata baadhi ya wanasiasa wasiokuwa Waislamu nao
wakisimama kidete dhidi ya mauaji hayo. Aidha, baadhi ya Waislamu nchini kwa
kujua ufaradhi wa kujihusisha na qadhia za Umma na kutambua Ummah wetu ni Ummah
mmoja wamekuwa wakipaza sauti zao kupitia vyombo vya habari, mihadhara,
makongamano, mikusanyiko ya nje ( picketing) na hata waliodiriki kutaka kufanya
maandamano lakini hawakufanikiwa kwa sababu nje ya uwezo wao. Wakati jitihada
hizo zote za ndani na nje zikijiri kulaani dhulma na ukatili wa Israili
Mheshimiwa Mufti na BAKWATA kwa masikitiko makubwa mko kimya kana kwamba hakuna
kinachoendelea.
Zaidi endelea kwa kubofya hapa....BARUA YA WAZI KWA MUFTI WA TANZANIA NA BAKWATA
Hakuna maoni
Chapisha Maoni