Mwenyekiti wa Chama hicho Hassan Dede
Na Mussa Augustine.
Chama Cha Madereva wa Malori na
Mabasi ya Masafa Marefu na Mafupi Tanzania ( TLDTA) kimesema kuwa uwekezaji wa
kuboresha Bandari ya Dar es salaam unaotaka kufanywa na serikali ya Tanzania
kwa shirikiana na serikali ya Dubai kupitia kampuni ya DP World utakua na
tija kubwa katika sekta ya usafirishaji.
Akizungumza na Waandishi wa
Habari Jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa Chama hicho Hassan Dede
amesema kuwa Serikali ya Dkt Samia Suluhu Hassan ina nia nzuri ya kukaribisha wawekezaji hivyo uwekezaji wa
kuboresha Bandari ya Dar es salaam kupitia DP World utasaidia kujitokeza
wafanyabiashara wengi wa Magari ya Usafirishaji wa mizigo nakwamba hali hiyo
itachangai kuongezeka kwa ajira za madereva.
" Mimi kama mwenyekiti jambo
hili ni kubwa kwetu kwani hakutakua na ucheleweshwaji wa mizigo tena,naipongeza
serikali kwa sasa mizigo mingi inapatikana katika Bandari yetu ukiacha Bandari
ya Msumbiji na Mombasa,Wafanyabiashara wa Zambia na Congo wanaiamini sana
Bandari ya Dar es salaam ,hivyo kama mradi huu wa DP World utatekelezwa sekta
ya Usafirishaji itaheshimika na Madereva watakua na maisha mazuri" Amesema
Hassan.
Amendelea kusema kuwa Mzigo unaotoka
Bandari ya Dar es salaam ni mwingi lakini unaposafirishwa kupelekwa Nchini
Zambia unakwama katika mpaka wa Zambia na Tanzania kutokana na miundombinu
ya Barabara za Zambia kuwa Mibovu hivyo ameishauri serikali ya Tanzania
kukutana na Serikali ya Zambia kuona namna ya kuiondoa changamoto hiyo.
Pia amesema kuwa kwa sasa madereva
wanasubiri mzigo kwa muda wa siku 1 hadi 2 nahiyo ni kutokana na kuwepo kwa
changamoto ya kimtandao wakati wa kuskani mzigo bandarini,lakini uboreshaji wa
Bandari ya Dar es salaam utakaofanywa na Kampuni ya DPW utasaidia kuondoa
mizigo kwa haraka zaidi.
Mwinjilisti wa Kimataifa Alphonce Temba
Kwa upande wake Mwinjilisti wa
Kimataifa Alphonce Temba ambaye pia ni Mfanyabiashara maarufu hapa nchini
amesema kwamba faini inayotozwa na Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) pamoja na
Wakala wa Barabara TANROAD pindi mafuta yanapomwagika wakati Malori
ya Usafirishaji wa mafuta yanapopata ajari ni uonevu mkubwa hivyo ameishauri
serikali kufanyia marekebisho sheria zinazosimamia kodi itokanayo na mafuta
yaliyomwagika Barabarani.
" Yaani mafuta
yamemwagika,halafu bado TRA na TANROAD wanatoza kodi ,huu sio ungwana
hata kidogo,naomba sana wabunge wajaribu kuona hili kwani ni uonevu wa hali ya
juu,na wafanyabiashara wa Malawi na Zambia wamekua wakilalamikia kodi hii
kwasababu kwao haipo,ipo hapa kwetu Tanzania,sasa tusipoangalia tutawafukuza
wafanyabiashara wa kigeni kwenye Bandari yetu" amesema Mwinjilisti wa
Kimataifa Temba.
Nakuomgeza kuwa" Mimi
kama Mwinjilisti wa Kimataifa, nina mambo 15 ambayo naweza kuishauri
serikali ili iweze kupata Mapato yatakayoisaidia serikali kutekeleza miradi ya
maendeleo na sio lazima tutegemee watu kutoka nje ,hivyo nipo tayari
kushirikiana na serikali kwa jambo lolote lenye kuleta maendeleo kwa Taifa.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni