DP KIMEMUOMBA RAIS. DKT SAMIA KUCHUKUA HATUA KUHUSU GHARAMA ZA MATIBABU MUHIMBILI.
Katibu Mkuu wa Chama Cha DP Abdul Mluya akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani).
Na Mussa
Augustine.
Chama Cha
Democratic Party (DP) kimemuomba Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuchukua hatua
kufuatia kuwepo kwa Vitendo vya kutozwa gharama kubwa kwa wagonjwa wanaotibiwa
katika Hospitali ya Taifa Muhimbili(MNH) hali ambayo inawafanya Wananchi
kushindwa kumudu gharama za matibabu.
Rai hiyo
imetolewa leo tarehe 28,2023 Jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu wa Chama hicho Abdul Mluya
wakati akizungumza na Waandishi wa habari ambapo amebainisha kuwa Waziri wa
Afya ameshindwa kuchukua hatua ya kuondoa changamoto hiyo nakuendelea kuwaumiza
Wananchi.
Amesema kuwa
imefika hatua baadhi ya Wananchi wamekuwa wakishindwa kuchukua miili ya
Wapendwa wao wanapofariki kutokana na kutozwa gharama kubwa ambapo ameiomba Serikali kuangalia kwa jicho la tatu gharama za Matibabu zisizo rafiki
kwa Wagonjwa.
“Suala la
kifo hua nila ghafla ,Maisha ya Watanzania yanatofautiana ,unapomtoza mamilioni
ya fedha mtu ambaye kafiwa na mpendwa wake na hana uwezo wa kulipa inamfanya
asusie maiti ,hivyo naiomba serikali iliangalie gharama hizi”amesema Mluya.
Nakuongeza
kwamba imefikia hatua pale Muhimbili imetengwa wodi maalumu kwa ajili
yakuwafungia wagonjwa ambao wameshindwa kulipa gharama za matibabu ili
wasitoroke ,yaani imetenga wodi hiyo kama Sero ni jambo la kusikitisha sana.
Katibu Mkuu
huyo wa DP ameongeza kuwa serikali isifanye afya ya Wananchi kua chanzo cha
kipato nabadala yake Waongeze tozo za kodi kwenye mambo ya Anasa kama vile
Pombe ,Kumbi za starehe(Nigth Clubs) na zinginezo.
“Ukilala
kwenye kitanda wodini kwa siku moja ni elfu thelathini(30,000) hapo bado gharama zingine
za huduma ,siku unatoka hospitalini ukipewa ile bili ina gharama kubwa
sana,ambapo kwa watanzania wa Maisha ya Kawaida inawaumiza sana ,sisi kama DP
tunaomba Waziri wa Afya ajitathmini na kama ameshindwa kazi Rais amsaidie
kupumzika”amesema
Hakuna maoni
Chapisha Maoni