WANANCHI KATA YA MZIMUNI WAMPA KONGOLE DIWANI WAO KWA KUWALETEA MAENDELEO.
Diwani Manifred Lyoto
Na Mussa
Augustine,
Baadhi ya
Wananchi wa Kata ya Mzimuni Manispaa ya Kinondoni Wamesema kuwa wanaridhishwa
na Utendaji kazi unaofanywa na Diwani wa Kata hiyo (CCM) Manifred Lyoto kwa
kuwa kuwaletea maendeleo katika sekta mbalimbali ikiwemo Sekta ya
Afya,Elimu,Michezo na Miundombinu ya Barabara na Maji.
Pongezi hizo
wamezitoa Juni 27 ,2023 wakati wakizungumza na waandishi wa habari
waliotembelea kata hiyo kwa ajili ya kuangalia utekelezaji wa Ilani ya Chama
cha Mapinduzi,ambapo kwa nyakati tofauti wananchi hao wamebainisha kuwa kwa
sasa kata hiyo imepiga hatua kubwa kimaendeleo.
Mmoja wa Wananchi hao anayefahamika kwa jina la Abdalah Kitumbi Mkazi wa Mtaa wa Mtambani amesema kuwa Diwani huyo ni Kiongozi wa Kuigwa kwani ameboresha sekta ya Elimu kwa kuhakikisha amejenga Uzio wa Shule ya Sekondari na Msingi Mzimuni ,ameweka Miundombinu ya kuwezesha Wanafuzni kupata chakula Shuleni,ameajiri walimu wa masomo ya sayansi hatua ambayo imechangia kuongezeka kwa ufaulu wa wanafunzi.
Picha ya Masufuria ya Kupikia Chakula
“Wazazi wanatoa elfu moja tu ya chakula kwa watoto wao ,Miundombinu mingine yote kama vile Jiko,Masufuria,Kontena la kuhifadhia chakula vyote amechangia Diwani kupitia fedha zake mwenyewe ili kuwapunguzia mzigo wa michango wananchi wa Mzimuni,kwakweli amekuwa akijitoa sana kutatua kero za wananchi”amesema Kitumbi. Picha ya Kontena la kuhifadhai Chakula
Picha ya Uzio wa sule katika shule ya Msingi na Sekondari MzimuniNae Irine
Mwakingila Mkazi wa Mtaa wa Mwanansari amesema kuwa Diwani huyo umesaidia kuboresha huduma za afya
katika Zahanati ya Mzimuni kutokana na kuoneza watumishi wengine wa afya kwenye
Zahanati hiyo ili kuhudumia wakazi wa maeneo hayo na kata jirani.
Ameendelea
kusema kuwa Diwani huyo ameanzisha Taasisi ya kutoa Mikopo isiyokua na riba kwa
Makundi ya Wajasiliamari ili kuwawezesha
kujikwamua kiuchumi,ambapo Taasisi hiyo iitwayo “Lyoto Foundation” itaanza kutoa
mikopo kuanzia Mwezi Julai mwaka huu.
Pia Kassim
Kinguyu Mkazi wa Mtaa wa Mtambani amesema kuwa Sekta ya Michezo imepewa
kipaumbele kwani tayari baadhi ya timu za Vijana zimepatiwa vitendea kazi vya
Michezo ikiwemo Jezi na Mipira,nakwamaba Diwani huyo yupo katika Mazungumzo na
wataalamu wa Soka kutoka Mataifa ya Nje kwa ajili ya kuwapeleka vijana wenye
vipaji kufanyiwa majaribio ya kucheza soka la Kimataifa.
Hata hivyo
kwa upande wake Diwani wa kata ya Mzimuni Manifred Lyoto amesema kuwa ameamua
kujitoa kuwasaidia Wananchi wa Kata hiyo kutokana nakwamba Serikali haiwezi
kufanya mambo yote kwa wakati Mmoja kwasababu inatekeleza Miradi mingi ambayo
inahitaji fedha nyingi.
“Serikali
ina mambo mengi yakufanya ,ina miradi mikubwa inayohitaji fedha,hivyo sisi kama
wawakilishi wa wananchi kama tunaweza kusaidia kupitia vyanzo vyetu vya binafsi
vya Mapato au kutafuta wadau wa kusaidia haina budi kufanya hivyo ili kuinga
mkono serikali katika kuwaletea Wananchi Maendeleo “amesema Diwani Lyoto
Nakuongeza
kuwa,”Nawaomba Wananchi wa Mzimuni wawe na mwamko mkubwa wa kupeleka watoto wao
shuleni kwani tumetatua changamoto zilizokuwepo,tushirikiane kwa pamoja kuleta
maendeleo kwenye kata yetu ,siokwamba tusubiri mpaka serikali ifanye”amesema
Kuhusu
utoaji wa Mikopo kupitia taasisi ya” Lyoto Foundation” Diwani huyo amesema kuwa
wanatarajia kuanza kutoa mikopo hiyo mwezi Julai Mwaka huu ili kuwasaidia
Wananchi wa kata hiyo wanaotaka kufanya ujasiliamari kwa lengo la kujikwamua
kiuchumi,
Hakuna maoni
Chapisha Maoni