DC KOMBA AWAOMBA WANANCHI WA GOBA KUJITOKEZA KWA WINGI KUCHANGIA DAMU KWA HIARI
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Hashimu Abdalah Komba
NA Mussa Augustine.
Mkuu wa Wilaya
ya Ubungo Hashimu Abdalah Komba amewaomba Wananchi wa Kata ya Goba Wilayani
humo kujitokeza kwa wingi katika zoezi la kuchangia Damu kwa hiari litakalofanyika katika
Senta ya Goba Juni 24 Mwaka huu.
DC Komba
ametoa rai hiyo wakati akizungumza na waratibu wa Kongamanohilo kutoka Taasisi
ya Hananja Compasion Foundation pamoja na Shirika la Misaada lakimataifa la
Marekani USID kupitia Mradi wake wa “Afya yangu”(Jhpiego USAID) walipo
mtembelea ofisini kwake kwa ajili ya kumpatia taarifa ya hatua ya maandalizi ya
zoezi hilo.
Aidha
amesema kwamba Wananchi wengi wanapoteza maisha kutokana na kukosa damu hivyo
elimu inapaswa kuendelea kutolewa ili jamii iwe na utamaduni wakujitoa kwa
ajili ya kuchangia Damu kwa hiari ili kuwezesha kuwepo na Damu ya kutosha
Mahospitalini.
“Damu ndio
Maisha,Damu haina Mbadala wake,haiuzwi hivyo mimi na wewe(Mwananchi)tunataka
Damu ,ni wakati sasa wa kuwa na tabia ya kuchangia Damu kwa hiari ili kuokoa
Maisha ya Dungu zetu pamoja na Wengine wanaopatwa na matatizo mbalimbali
ikiwemo ajali”amesema DC Komba
Nakuongeza kuwa”Wakina Mama wajawazito wanapoteza maisha wakati wa kujifungua kutokana na kukosa Damu,nawaomba sana Wananchi wa Goba na maeneo mengine wajitokeze jumamosi ya tarehe 24 mwezi huu wa sita wachangie Damu kwa hiari ili tuwe na akiba ya Damu ya kutosha Mahospitalini.
Mratibu wa Damu Salaama Manispaa ya Ubungo Analimi Machalo
Kwa upande wake Mratibu wa Damu Salaama Manispaa ya Ubungo Analimi Machalo amebainisha kuwa Wilaya hiyuo imejiwekea lengola kukusanya Uniti 311 kwa mwezi,huku kwa mwaka imepanga kukusanya Uniti 3731 za Damu,nakwamba hadi sasa Wilaya hiyo imekusanya Uniti 1505 sawa na asilimia 40.
Aidha
ameongeza kuwa siku ya zoezi hilo litakalofanyika Goba wanatarajia kukusanya
Uniti 300 za Damu hivyo amewaasa Wananchi kujitokeza kwa wingi ili kuchangia
Damu kwa hiari nakuwezesha kufikia malengo waliojiwekea nakuwa na Damu ya
kutosha Mahospitalini.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni