IRINE UWOYA AMPONGEZA DKT.SAMIA KUFANYA MAGEUZI MAKUBWA SEKTA YA KILIMO.
Mwigizaji wa Bongo Movie Irine Uwoya amempongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kufanya Mageuzi makubwa kwenye sekta ya Kilimo.
Pongezi hizo amezitoa leo Januari 26,205 Jijini Dar es salaam wakati akitambulisha mradi mpya ujulikanao kama " Jembe ni Mama" ambao umelenga kuhamasisha wanawake wakulima Nchini kufanya kilimo Cha kisasa kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi.
Uwoya ambaye ni Mwenyekiti wa mradi huo ameendelea kusema kuwa ameamua kuanzisha Mradi huo kutokana na yeye binafsi kuwekeza kwenye sekta ya Kilimo ambapo amefanikiwa kufanya kilimo Cha Tanagawizi pamoja na Mpunga huko Mbarali Mkoani Mbeya.
Amesema kuwa kwa Sasa sekta ya Kilimo imepiga hatua kubwa kutokana na Serikali kuwekeza kwenye sekta hiyo kwa kuwezesha wakulima kupata pembejeo za kilimo,Zana Bora za Kilimo pamoja na Mikopo ya kuwawezesha katika kilimo.
" Toka nianze kujihusisha na kilimo Mwaka 2018 ,nimeona Mapinduzi makubwa sana ndani ya sekta ya kilimo,namshukuru sana mama yetu na Rais Wetu Dkt Samia,pamoja na Waziri wa Kilimo Hussein Bashe kwa jitihada hizi wanazizifanya katika kuleta Mapinduzi ya Kilimo" amesema
Nakuongeza kuwa Sekta ya Kilimo ni muhimili muhimu katika pato la Taifa,nakwamba Serikali imekuwa ikiweka mazingira rafiki katika kukuza sekta hiyo kwa kuweka jitihada muhimu ikiwemo kusimamia kilimo cha kisasa, kutoa pembejeo za kutosha,kutafuta masoko ya uhakika kwa ajili ya wakulima kuuza mazao yao,pamoja na kutoa Mikopo kwa wakulima wadogo.
Amesema kwamba asilimia 67 ya wanawake ndani ya familia wanajihusisha na kilimo,asilimia 29 ni wanaume ndani ya familia wanajihusisha na kilimo,pia asilimia 4 pekee ni wanawake na wanaume ndani ya familia wasiojihusisha na uzalishaji wa aina yoyote.
"Jembe ni Mama" ni kampeni ambayo nimeanzisha kwa ajili ya kusaidia Wizara ya Kilimo kuwa na kilimo bora chenye maslahi kwa wanawake wakulima nchini Tanzania" amesema Uwoya.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni