Zinazobamba

TLDTA : AJARI ZA MABASI YA ABIRIA ZINASABABISHWA NA WAMILIKI WA MABASI WENYEWE

 Mwenyekiti wa Chama Cha Madereva  wa Malori na Mabasi Tanzania(TLDTA) Hassan Dede 

Na Mussa Augustine.

Mwenyekiti wa Chama Cha Madereva  wa Malori na Mabasi Tanzania(TLDTA) Hassan Dede amesema kuwa sababu kubwa inayosababisha kutokea kwa ajari ya Mabasi ya Abiria na kusababisha vifo kutokea ni Wamiliki wa Mabasi hayo kushindwa kulipa maslahi stahiki madereva Wao pamoja na kufanya biashara hiyo kwa ushindani.

Kauli hiyo ameitoa leo Julai 4 ,2023 jijini Dar es salaam  wakati akizungumza na Jamhuri ikiwa ni siku moja baada ya Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Ardhini  (LATRA) kusitisha safari za kuanzia  saa tisa usiku  hadi saa  kumi na moja  alfajiri za Kampuni ya Mabasi ya NEW FORCE  kwa madai kuwa imesababisha ajari nyingi kwa kipindi kifupi tangu kuruhusiwa kwa safari hizo.

Amesema kuwa Madereva wengi wenye taaluma na uzoefu mkubwa wamekuwa wakinyang”anywa Mabasi na Matajiri wao kutokana na sababu kuwa wanaendesha kwa mwendo wa taratibu ,hivyo matajiri hao wanawapa madereva wasio na uzoefu wala sifa ambao wanaendesha kwa mwendo wa kasi hali ambayo inasababisha ajari kutokea.

" Wamiliki wengi wa Mabasi wana mikopo Benki hivyo wanafanya biashsara kwa ushindani ,ukionekana dereva unaendesha taratibu kwa kuzingatia sheria za usalama barabarani basi huna kazi tena ,anatafutwa dereva mwingine  ambaye ataendesha kwa mwendo wa kasi hali ambayo imekuwa ikichangia sana kutokea kwa ajari” amesema Dede.

Amesema kuwa Mwarobaini wa ajari hizo ni kuhakikisha Madereva wamejiunga kwenye Chama Cha Madereva wa Malori na Mabasi ili kuweza kuwadhibiti kwa urahisi wale wote Madereva wasio na sifa wanaotumiwa na wamiliki wa Mabasi ya abiria.

“Tuache biashara huria kwenye Sekta ya Usafirishaji wa abiria kwani ina gusa maisha ya Watu,tunaomba sana wamiliki wa mabasi ya abiria wajitathmini” amesema Dede kwa msisitizo mkubwa.              

Hata hivyo ameongeza kuwa Kwa niaba ya Madereva wenzake ameipongeza serikali ya Dkt Samia Suluhu Hassan kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani  kuleta mpango wa Madereva kurudi shuleni kusoma ili wapate taaluma itakayowawezesha kupata Leseni zinazoendana na Madaraja waliyosomea.

“Rais Dkt Samia amekuwa akisisitiza kwamba amechoka kutoa rambirambi kwa ajili ya vifo vitokanavyo na ajari ,hivyo ni wakati sasa Wamiliki wa Mabasi watumie Madereva Wenye sifa lakini pia wawalipe Stahiki zao kwa mujibu wa sheria”amesema.

 Nakuongeza kuwa “Wamiliki wengi ni watunga sera(Wabunge)ndio maana baadhi ya Kampuni za Mabasi zinapuuza baadhi ya taratibu za Usalama Barabarani.

Kwa Mujibu wa LATRA kwenye Mkutano na Waandishi wa habari Julai 3,203 jijini Dar es salaam,Kampuni ya Mabasi ya Abiria ya NEWFORCE imesitishiwa safari zake za usiku kuanzia saa tisa hadi saa kumi na moja alfajiri ,nakwamba itandelea na safari zake za kawaida kuanzia saa kumi na mbili alfajiri na kuendelea.



Hakuna maoni