RAIS WA HUNGARY KATALIN VOVAK ANATARAJIWA KUWASILI NCHINI TANZANIA KWA ZIARA YA KIKAZI
Na Mussa Augustine
Rais wa Hungary Katalin Novak anatarajiwa Kuwasili leo na kufanya ziara yake Nchini Tanzania kuanzia July 17 hadi 20 ,2023 ziara hiyo ikiwa ni matokeo ya jitihada ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan za Kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na Mataifa mengine.
Hayo
yamesemwa leo Julai 17 ,2023
na Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Stergomena Tax wakati akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar es salaam nakubainisha kuwa kufanyika kwa ziara
hiyo ni moja ya jitihada za Rais
Dkt Samia Suluhu Hassan za kuimarisha uhusiano wa kimataifa na
kikanda.
Aidha Waziri Tax amesema ushirikiano uliopo
kati ya Tanzania na Hungary ni kuinua sekta ya Elimu kwa kutoa nafasi za
mafunzo mbalimbali katika nyanja mbalimbali hususania katika sayansi na
Teknolojia.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Stergomena Tax
Mkurugenzi
wa kitengo cha habari wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika
Mashariki Balozi Mindi Kasiga amesema ziara hiyo imekuja
kutokana na sera mpya nchini Hungary Kwa nchi za Afrika inayolenga
Kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi ambao ulianza kutekelezwa na Taifa
hilo miaka michache iliyopita huku akibainisha kuwa uhusiano wa Tanzania
na Hungary ni mzuri tangu enzi za muungano wa Sovieti na kupitia ziara hiyo
uhusiano utaimarika .
Mkurugenzi wa kitengo cha habari wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mindi Kasiga
Hakuna maoni
Chapisha Maoni