Zinazobamba

Mwenyekiti wa UWT na Makamu wake wafanya Ziara ya kutembelea Bandari ya Kilwa

Mwenyekit wa UWT Taifa Ndugu Mary Chatanda na Makamu Mwenyeki wa UWT Ndg. Zainab Shomari wakiambatana na Kamati ya Utekelezaji UWT wametembelea mradi wa Bandari ya Kilwa.

Aidha Kamati hiyo imeridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa Bandari hiyo huku Mwenyekit wa UWT Taifa Ndugu Mary Chatanda akiwataka wakandarasi kutekeleza mradi huo kwa wakati kwani wananchi wa Kilwa wanategemea kunufaika na mradi huo.

Sambamba na hilo akautaka uongozi wa Bandari kuwa na usawa kwenye suala la ajira kwa jinsia zote kwa wanawake na wanaume kwani malengo ya Serikali ni kuhakikisha kila mwananchi ananufaika na matunda ya Nchi yake.

Chatanda akamalizia kwa kusema.

"Kuna watu wana nia mbaya na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Ndugu Samia Suluhu Hassan kwa kupotosha jamii, kwamba Bandari imeuzwa niseme Ndugu wananchi msiwasikilize hao ni matapeli"

Ameyasema hayo Leo tarehe 13 Julai,2023 alipoambatana na Kamati ya Utekelezaji UWT mara baada ya ukaguzi wa Bandari ya Kilwa Mkoani Lindi.

Hakuna maoni