JAJI MTUNGI :VYAMA VYA SIASA ZINGATIENI MAELEKEZO YA KISHERIA YANAYOTAKIWA KUFUATWA.
Na Mussa Augustine.
Msajili wa
Vyama Vya saiasa Nchini Jaji Francis Mutungi amevitaka Vyama vya siasa
kuzingatia maelekezo ya kesheria yanayotakiwa kufanyiwa marekebisho ili
kuvifanya vyama hivyo kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria.
Agizo hilo
amelitoa leo Jinini Dar es salaam wakati akifungua semina ya siku mbili ya
viongozi wa vyama vya siasa Nchini,ambapo amesema kuwa Ofisi yake imekua
ikiendesha zoezi la kuvihakiki vyama hivyo Kila mwaka ili kujiridhisha kama
vinaendesha majukumu yake ya kitaasisi kwa kukidhi matakwa ya kisheria.
"Kabla
ya kufanya uhakiki wa vyama hivi vya siasa kwa mwaka huu ,leo tunatoa semina
Kwa viongozi wa vyama vya siasa kabla ya kufanya usajili wa vyama kumi na
nane(18) vingine ambavyo vimeomba kusajiliwa,tukimaliza zoezi hili
tunafanya zoezi la uhakiki wa vyama hivyo ili kubaini mapungufu ya kisheria
yaliyopo nakuvipa muda wa kuondoa kasoro hizo" amesema Jaji Mutungi
Aidha ameongeza kuwa Vyama Vya Siasa vimekua vikipata hati chafu kufuatia ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa hesabu za Serikali(CAG) kutokana na kushindwa kutunza vizuri kumbukumbu za matumizi ya fedha ndani ya taasisi hizo hivyo kupitia uhakiki huo umelenga kuvifanya vijiendeshe kama taasisi za umma Kwa kuzingatia utunzaji mzuri wa kumbukumbu za matumizi ya fedha.
Kwa upande wake Mwenyekiti Taifa wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania( TCD) Profesa Ibrahim Lipumba amesema kuwa Sheria ya vyama vya siasa imetoa maelekezo ya kuhakikiwa Kila mwaka ili kuangalia mambo mbalimbali ikiwemo rejista ya wananchama,ripoti ya fedha pamoja na Usajili wa bodi ya wadhamini ya chama,hivyo lengo kubwa ni kuvisaidia vyama vya siasa kutekeleza wajibu wake kwa kufuata Sheria.
"Semina hii niya kikazi ,kwani imetukutanisha hapa ili kukumbushana mambo ya Msingi ya kusimamia katika taasisi zetu za vyama vya siasa,amesisitiza Profesa Lipumba ambaye pia ni mwenyekiti Taifa wa Chama Cha Wananchi ( CUF
Nae mwenyekiti Taifa wa Chama Cha Alliance for Democratic Change( ADC) Hamad Rashid amebainisha kuwa vyama vya siasa vimekua vikipata hati chafu kutokana na kukosa elimu ya namna ya kutunza kumbukumbu za matumizi ya fedha hivyo kupitia semina hiyo ambayo inatolewa na ofisi ya Msajiri wa Vyama vya siasa itasaidia kuondokana na hati chafu za CAG.
Hata hivyo
Naibu Katibu Mkuu CCM Bara Annamringi Macha amesema kwamba
vyama vya siasa vipo kwa ajili ya kufanya kazi za maslahi ya Taifa ,hivyo Nia
ya msajili wa vyama vya siasa kuvihakiki ni kuvifanya vikidhi matakwa ya
kisheria huku akisisitiza kuwa CCM kimekua makini katika utunzaji wa ripoti za
matumizi ya fedha ndiyo maana muda mrefu hakijata hati chafu kutoka Kwa CAG.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni