Zinazobamba

MWAKIPOSA AMSHUKURU RAIS SAMIA UTEKELEZAJI MIRADI DOVYA.

Na Moshi Said

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Dovya Boko jijini Dar es salaam Lazarus  Mwakiposa amempongeza Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa utekelezaji wa mradi wa Barabara Kwa kiwango Cha lami mtaani kwake.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Dovya Boko jijini Dar es salaam Lazarus  Mwakiposa.
Akizungumza na waaandishi wa habari jijini Dar es salaam waliotembelea mradi huo amesema yeye pamoja na Wananchi wote wa Mtaa wa Dovya  wanajivunia kuwa na barabara hiyo itakayokuwa na kiwango Cha lami kutokana na jitihada binafsi alizozifanya za ufuatiliaji na usimamizi wa Barabara hiyo inayojengwa na wakala wa Barabara mijini na vijijini nchini TARURA.

Mwenyekiti huyo ambaye  pia ni Mwenyekiti wa wenyeviti wa Serikali za mitaa wilaya ya kinondoni na Makamu Mwenyekiti wa wenyeviti hao Mkoa wa Dar es salaam amesema awali kabla ya barabara hiyo kujengwa kwa kiwango hicho cha lami ilikuwa na kero kubwa kwa waendesha magari na pikipiki ambao walilalamikia vyombo vyao hivyo vya moto kuharibika mara kwa mara kutokana na uchakavu na ubovu wa miundombinu ya Barabara hiyo.

"Kwa kweli hii barabara ilikuwa na changamoto sana siku za nyuma ilikuwa ikipitika kwa tabu na kuharibu magari ya Wananchi kulikopelekea malalamiko mengi ofisini kwangu" amesema Mwakiposa.
Mwakiposa amesema mara tu baada ya kukamilika Kwa barabara hiyo kutaleta tija kwa Wananchi wake wanaotumia barabara hiyo ikiwemo kwa shughuli za uzalishaji uchumi, kusafirisha wagonjwa na watembea Kwa miguu.

Amesema ujenzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 2.7 inaanzia eneo la National Housing hadi wazo Magereza  ikienda sambamba na ujenzi wa daraja linalounganisha barabara hiyo linalogharimu shilingi milioni 400.

Hakuna maoni