DIWANI LYOTO AISHAURI SERIKALI KUHUSU KUDHIBITI USHOGA.
Diwani wa Kata ya Mzimuni Manfred Lyoto
Na Mussa Augustine.
Diwani wa Kata ya Mzimuni Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Manifredy Lyoto ameishauri Serikali kutunga sheria itakayodhibiti vitendo vya ushoga pamoja na watoto wadogo Kuishi shule za bweni kwani kunahatarisha maadili ya Taifa.
Diwani Lyoto amesema hayo jijini Dar es salaam Machi 9 ,2023 wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi nakusema kwamba kuibuka kwa taarifa za kuwepo kwa vitendo vya kulawitiana kwa watoto mashuleni pamoja na ushoga inasababisha kupotea kwa maadili ya kitanzania na kiafrikahivyo lazima vitendo hivyo vikemewe.
“Nisuala ambalo nila ajabu hatukudhani kama litatokea lakini mpaka sasa tunavyoongea lipo,hivyo tuwaombe viongozi wa dini waongeze bidii kuwafundisha waamini wao na kujua ubaya wa kitendo cha ushoga kwenye jamii"amesema
Nakuongeza kwamba "Nasisi kwenye jamii yetu mfano mimi kwenye kata yangu nimekua nikiwaita wananchi tunajadili kuhusu masuala ya maadili ya watoto wetu ,na kama atabainika mtoto anafanya vitendo vya uhalifu ikiwemo ushoga tutamchukulia hatua kali sana .
Aidha amesema kwamba suala hilo la ushoga lichukuliwe kwa uzito nakwamba Tanzania kama Taifa lazima kuamka nakuhakikisha matendo machafu yanadhibitiwa ili kulinda tamaduni zetu,pia ameshauri kutumia wataalamu kutoka vyuo vikuu kufanya utafiti ili kubaini chanzo cha tatizo hilo ili kuchukua hatua.
Hata hivyo amewaomba Wazazi pia kutekeleza wajibu wao wa malezi kwa watoto nakuacha tabia za kupeleka shule za bweni watoto wa shule za msingi kwani kufanya hivyo hawapati malezi muhimu ya wazazi na wengine kuanza kufundishwa tabia mbaya ikiwemo vitendo vya kulawitiana nakupelekea kuwa mashoga.
Katika hatua nyingine
Diwani Lyoto amezungumzia miaka miwili ya kuwepo madarakani Rais Dkt Samia Suluhu Hassan nakusema kuwa
uongozi wake umetukuka kwani ameendeleza vizuri miradi mikubwa ya kimkakati
iliyoachwa na mtangulizi wake Hayati Dkt Jonh Magufuli aliyefariki Dunia mwezi
Machi ,2021
Amesema kwamba Rais Drk Samia ameonyesha ukomavu wake katika uongozi kutokana na kutekeleza miradi mbalimbalj ya Sekta ya Elimu,Afya,Miundombinu ya Barabara ,Maji,Kilimo,Nishati ya Umeme,nakwamba kuwa mwanamke hakumaanishi chochote kuwa hawezi kuongoza.
"Jana (Machi 8 siku ya wanawake duniani) amevunja rekodi ya kuhudhuria mkutano wa Baraza la Wanawake la Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, ( BAWACHA) ameonesha tofauti za kiitikadi ,amefanya ambayo wanaume viongozi waliopita hawakufanya,kwasasa hali ya Demokrasia imeanza kua tulivu nchini,amesema Diwani Lyoto.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni